Nini maana ya mstari huu “Hatukuja na kitu duniani, na tena hatuwezi kutoka na kitu? (1 Timotheo 6:7)

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

1 Timotheo 6:7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; 

JIBU: Mstari huo unakuhusu wewe, mimi, mama yako, baba yako, mtoto wako, ndugu zako, Rais wako, waziri wako, mafalme wako, malkia wako, mume wako, mke wako, nabii wako, mchungaji wako, askofu wako, na mwanadamu yo yote yule mwenye mwili unayemfahamu wewe hapa duniani, bila kujali yeye ni nani (maskini au tajiri, mnyonge au hodari), wote hatukuja na kitu hapa duniani na wala hakuna tunachomiliki hapa duniani (hata sisi wenyewe si mali yetu wenyewe).

Zaburi 24:1 NCHI NA VYOTE VIIJAZAVYO NI MALI YA BWANA, DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE.

Hiyo ardhi unayoilima hukuja nayo, umeikuta hapa hapa duniani, huyo kijakazi uliyenaye nyumbani kwako hukuja naye, umemkuta hapana duniani, huyo mume au mke uliye nae umemkuta hapa duniani, baba au mama ulio nao wote umewakuta hapa duniani, hao ndugu, marafiki, na maadui, wote umewakuta hapa hapa duniani, harikadharika na watoto zako ulionao pia umepewa na Mungu, na ukifa unaenda zako na kuwaacha hapa hapa na hakuna utakachoondoka nacho, hiyo nyumba yako ya udongo au ya manyasi ukifa unaiacha hapa hapa duniani, hilo ghorofa lako la kifahari ukifa unaliacha hapa hapa duniani, pesa zako benki, baiskeli yako nyumbani, gari lako, cheo chako, shahada yako n.k, vyote tutaviacha hapa hapa duniani. 

1 Timotheo 6:7 Kwa maana HATUKUJA NA KITU DUNIANI, TENA HATUWEZI KUTOKA NA KITU; 

Sasa ili tuelewe vizuri, inabidi tumtazame mtu wa kwanza kabisa kuumbwa na kuwepo duniani ambaye ni Adamu, ukisoma maandiko, utagundua kuwa, Adamu hakuleta kitu chochote kile hapa duniani, Mungu ndiye aliyefanya kila kitu, alimfanyia msaidizi kutoka katika ubavu wake n.k, na alipokufa, hakuna chochote kile alichoondoka nacho, hivyo ndivyo itakavyokua na kwetu sisi pia tutakapokufa.


Lakini hiyo sio shida, shida ni kwamba, tunaondoka hapa duniani katika hali gani na hatma ya roho zetu itakuwa ni wapi? Kwa sababu miili yetu itairudia ardhi tutakapo kufa (Mwanzo 3:19), lakini roho zetu zina sehemu mbili za kwenda, Jehanam kama tusipo mwamini na kumtii Yesu Kristo (Luka 12:5), au peponi kama tukifa ndani ya Kristo (Wafilipi 1:23), kama Bwana mwenyewe alivyosema..

Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. YEYE ANIAMINIYE MIMI, AJAPOKUFA, ATAKUWA ANAISHI; 

Je! Vitu ambavyo hukuja navyo duniani na utaviacha hapa hapa siku utakayokufa ndio visabishe roho zetu kwenda Jehanam? Je! Vitu hivyo ndivyo vitufanye kushindwa kumtii Bwana na injili yake? Je! Ni huyo mke wa mtu unayeishi nae ambaye hukuja nae hapa duniani ndiye anayekuzuia kuitii injili ya Kristo na kwenda Jehanam kwa sababu ya uzinzi? Je! Ni huyo mume wa mtu unayeishi nae ambaye hukuja nae duniani ndiye anayekuzuia kuitii injili ya Kristo na kwenda Jehanam kwa sababu ya uasherati? Je! Ni hiyo kazi ya uuzaji bangi na madawa ya kulevya? Ni hiyo kazi ya ujambazi na uporaji? Ni hiyo kazi ya uuzaji pombe na sigara ndiyo inayokuzuia kumtii Kristo na injili yake? Ni hiyo kazi ya bar? Ni hiyo kazi inayokulazimisha kuvaa mavazi ya kikahaba mwanamke? Ni hao marafiki wapenda anasa amabo hukuja nao ndio wanaokufamya uende Jehanam kwa kushindwa kumtii Mungu, je! Ni huyo nabii wako wa uongo uliyemkuta hapa duniani? Ni hilo dhehebu lako la uongo lenye mafundisho potofu? Ni hilo dhehebu lako linalokufundisha KUWAOMBA WAFU na KUABUDU SANAMU (machukizo kwa Bwana), ni hiyo taasisi yako ya dini ya uongo inayokufundisha hakuna moto wa milele? Ni hilo dhehebu lako linalokufundisha ukifa hakuna kinachoendelea? Ni hiyo taasisi yako inayopinga ubatizo sahihi na maagizo ya Bwana?


Ndugu, vitu tutakavyoviacha hapa ambavyo hatukuja navyo visitufanye tuukose uzima wa milele, tujikane nafsi zetu tuitii injili ya Bwana.

Marko 9:43 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; 

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.


Mada zinginezo:

Itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni.


Bwana alimaanisha nini aliposema “Heri ayawe yote asiyechukizwa nami?” (Mathayo 11:6)


NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI.


Ni mambo ya nyumba ipi ambayo mfalme Hezekia aliambiwa kuyatengeneza? (Isaya 38:1)


Ni thawabu gani inayozungumziwa katika (Mathayo 6:16)?


Bado Bwana Yesu anasema nawe kwa mifano?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *