Kwenye taifa la Israeli katika torati, iliagizwa kuuawa kwa nabii yo yote yule atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina la Bwana, yaani nabii atakayenena neno kwa mawazo yake, mtazamo wake na hisia zake, halafu akasema ni neno la Bwana au ni Bwana Ndiye Aliyesema, au atakayenena neno ambalo Bwana hakuliagiza bali kulingana na hisia zake na akili zake na kudanganywa kwake (yaliyopotoka), Sharti ilikuwa ni lazima AUAWE (ndivyo torati ilivyoagiza).
Kumbukumbu La Torati 18:20 LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, au atakayenena katika jina la miungu mingine, NABII YULE ATAKUFA.
Soma tena.
Kumbukumbu La Torati 13:5 NA YULE NABII, au yule mwotaji wa ndoto, NA AUAWE, KWA KUWA AMESEMA YALIYOPOTOKA JUU YA BWANA, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako.
(Hii ikiwa inatupa picha halisi ni kwa jinsi gani Bwana anavyochukizwa na manabii wa uongo)
Lakini kama tunavyojua, Torati ni kivuli cha agano jipya (Waebrania 10:1), na yote yaliyonenwa kwenye torati ni lazima yatimie na kwamwe torati haiwezi tanguka, kama ilivyoandikwa.
Luka 16:17 Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, KULIKO ITANGUKE NUKTA MOJA YA TORATI.
Hivyo basi ni wazi kuwa, andiko hilo la torati la KUUAWA kwa manabii wa uongo wanaonena kwa hisia zao na mawazo yao binafsi na kusema ni neno la Bwana, ni lazima litimie juu yao, na kuuwa kwenyewe au kifo chenyewe sio kingine zaidi ya MAUTI YA PILI KWENYE LILE ZIWA LA MOTO NA KIBERITI
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI.
Katika siku hivi za Mwisho, Bwana alitabiri manabii wengi wa uongo kutokea (yaani Mitume, manabii, wainjilisti wachungaji, na waalimu), na kuwadanganya wengi (kwa kusema maneno ambayo Yeye Mungu Hakuyaagiza, yaliyo kinyume na kweli yake na injili yake), hivyo kama na wewe unayesoma ujumbe huu ni mmoja wapo wa hao unapaswa ubadilike na uyaseme yale yaliyosemwa kweli kweli na Bwana (Rejea maandiko matakatifu), vinginevyo andiko hilo hilo la torati litatimia juu yako.
Wewe unayejiita mchungaji, mwalimu, Mwinjilisti, nabii, mtume, askofu n.k, unayewaambia watu neno la Bwana (injili ya Mungu) kulingana na mitazamo yako na hisia zako, kulingana na mawazo yako na uongo wako uliouchukua kutoka kwenye filosofia na theologia, na kusema kuwa hivi ndivyo anenavyo Bwana, hivi ndivyo alivyosema Bwana, tambua kuwa unapaswa ubadilike na uyaseme yale yaliyosemwa kweli kweli na Bwana (Rejea biblia yako), vinginevyo nabii wewe UTAKUFA kwa mauti ya pili kwenye ziwa la moto na kiberiti kwani Bwana ameshatoa OLE.
Ezekieli 13:2 Mwanadamu, tabiri juu ya manabii wa Israeli wanaotabiri, uwaambie wanaotabiri KWA MIOYO YAO WENYEWE, Lisikieni neno la Bwana;
3 Bwana MUNGU asema hivi; OLE WAO MANABII WAJINGA, WANAOIFUATA ROHO YAO WENYEWE, wala hawakuona neno lo lote!
Bwana akubariki, Shalom.
Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.
+255652274252/ +255789001312
Mada zinginezo:
FUNZO KATIKA HABARI YA MFALME AHABU NA NABII MIKAYA
Nini maana ya mstari huu “unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu” (2 Petro 2:21)
MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 10)
DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.