Jina la Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele, karibu katika kujifunza maneno ya uzima ya Mungu Wetu Yesu Kristo, ili tuyajue mapenzi yake na kujitahidi kwa bidii kuwa wakamilifu na bila lawama mbele zake katika ile siku atakapokuja kuwanyakua watakatifu wake (1 Wathesalonike 5:23)
Biblia inasema hivi katika…
Matayo 24:26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.
27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Kabla ya kuja kwake Mwana wa Adamu kuwanyakua watakatifu wake kwa kufumba na kufumbua (kama umeme) Bwana alisema kuwa, kutatokea mafundisho mengi ya uongo yatakayoletwa na makristo na manabii wengi wa uongo (manabii wa uongo wanaweza kuwa waalimu wa uongo, wachungaji wa uongo, maaskofu na viongozi wote wa dini wa uongo) na hivyo Bwana alituambia tusiwasikilize kamwe watu hao. Wakituambia Kristo yupo huku au hapa tusisadiki kamwe, bali TUKAE HAPO HAPO TULIPO HADI ATAKAPO KUJA.
Sasa zamani kabla ya kuzaliwa upya, nilikuwa nadhani kwamba, natakiwa nikae na kubaki hapo hapo nilipo hadi Kristo atakapokuja na sitakiwi kwenda kokote kule sawasawa na neno hili la Bwana
Matayo 24:26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.
Lakini sivyo, na ninataka nikwambie na wewe ndugu yangu ambaye pengine ulikuwa una waza hivyo, Bwana hakumaanisha ukae hapo katika hilo dhehebu lako, bali, alimaanisha UKAE KATIKA NENO LAKE kwa sababu maneno hayo aliwaambia wanafunzi wake wa wakati huo ambao walikaa katika neno lake, kwamba mtu yoyote akitokea na kuwaambia maneo mengine au mafundisho mengine ambayo hayakutoka kwake, basi, wasisadiki wala kuwafuata, kwani hao ndio manabii, waalimu, mapadre, na wachungaji wa uongo.
Ukijiona upo mahali ambapo ulibatizwa kwa kunyunyuziwa maji, kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na tena ulikuwa mtoto mchanga wala hujitambui, basi fahamu kuwa, ulishapotezwa muda sana na hayo mafundisho ya uongo, muulize huyo kiongozi wako mbona mitume waliobatizwa na kubatiza kwa Jina la Yesu Kristo?
Matendo Ya Mitume 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Na Yesu aliwaambia mitume wake kuwa, atakayewasilikiza ninyi, ananisikiliza mimi? Hivyo tukiyasikiliza mafundiaho ya mitume wa Yesu, tumemsikiliza yeye, na tukiyakataa tumemkataa yeye?
Luka 10:16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
Dada/mama, ukijiona upo sehemu ambayo unaruhusiwa kuvaa vimini, suruali, make-up, mawigi, kucha bandia, hereni, n.k na wala hukemewi, na kibaya zaidi unaambiwa hakuna shida na wala sio dhambi, na huambiwi kufunika kichwa chako wakati wa ibada mwanamke, basi fahamu kuwa ulishayasadiki haya mafundisho ya uongo muda sana.
Ukijiona upo kwenye kanisa ambalo mchungaji wako au askofu wako ni mwanamke, basi fahamu kuwa upo chini ya mafundisho ya manabii wa uongo, haijalishi huyo mchungaji wako anajua kuhubiri kama Paulo.
Ukijiona upo kwenye kanisa ambalo hukemewi kufuga rasta zako hizo wewe mwanume, wala kiduku chako hicho kichwani, wala milegezo yako, na ulevi na mwanamke unayeishi nae wakati hujamtolea mahari wala kufunga nae ndoa, basi fahamu kuwa, ulishayasadiki hayo mafundisho ya manabii na waalimu wa uongo muda sana.
Ukijiona upo kwenye kanisa ambalo, unafundishwa kumuomba Maria, au Yosefu, na kuyachukua masanamu yao na kuzunguka nayo nyumba kwa nyumba, au unainamia sanamu la Maria lenye macho lakini halioni na masikio lakini halisikii, au unasisitizwa juu ya mafuta ya upako n.k basi, fahamu kuwa ulishayasadiki na kuchukuliwa na mafundisho ya uongo, haijalishi huyo kiongozi wako ana upako kiasi gani?
Hivyo toka huko leo na anza kulisoma neno la Mungu na mafundisho ya mitume wake, na udumu katika hayo ili Mwana wa Adamu ajapo akukute unadumu katika hayo.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Bwana akubariki, Shalom.
+255652274252/ +255789001312
Mada zinginezo:
LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.
Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?
Ni maneno yapi ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo? (Kulingana na 1 Timotheo 1:18)
Ni tabia ipi ya Uungu tutakayoshiriki (kulingana na 2 Petro 1:4)