Je! Andiko la (Wafilipi 4:3), linatoa ruhusa kwa wanawake kuchunga makanisa, kusimamia makanisa, na kusimama madhabahuni ili kuhubiri na kufundisha?

SWALI: Je! Ni kweli andiko la (Wafilipi 4:3), linatoa ruhusa kwa wanawake kuchunga na kusimamia makanisa ya Mungu Kwa sababu ya wanawake Euodia na Sintike walioishindania injili pamoja na Mtume Paulo huko Filipi?

Wafilipi 4:2 Namsihi EUODIA, namsihi na SINTIKE, wawe na nia moja katika Bwana. 

3 Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie WANAWAKE HAOKWA MAANA WALIISHINDANIA INJILI PAMOJA NAMI, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima. 

JIBU: Andiko hilo halijatoa ruhusa yo yote ile ya wanawake kusimama madhabahuni katika kanisa la Kristo na kuhubiri au kufundisha, na wala halijatoa ruhusa ya wanawake kusimamia na kuchunga makanisa ya Mungu kwa sababu kazi ya usimamizi na uchungaji wa kanisa la Mungu (au watu wa Mungu), ni kazi ya UKUHANI, (na ndiyo aliyokuwa akiifanya mtume Paulo)

Warumi 15:15 Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu, 

16 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, NIIFANYIE INJILI YA MUNGU KAZI YA UKUHANI, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu. 

Na katika maandiko matakatifu hakukuwa na hakuna Kuhani yo yote yule wa Mungu ambaye ni mwanamke, (hata Baali hawakuwa na makuhani wa kike katika maandiko). 


Ndivyo ilivyo na sasa pia katika agano jipya kuwa, wanawake wanayosehemu yao ya utumishi katika kuihudumia injili ya Kristo lakini si katika ukuhani (yaani Usimamizi na uchungaji wa makanisa), na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wanawake EUODIA na SINTIKE waliofanya kazi na mtume Paulo, haina maana na wao walikuwa mitume, maaskofu, wachungaji, au wasimamizi wa makanisa ya Mungu, la! Hasha.


Katika Kanisa, mwanamke anaweza nena kwa lugha, mwanamke anaweza kuwa nabii na kutabiri, mwanamke anaweza tumiwa na Roho kufikisha ujumbe fulani wa Mungu katika kanisa, mwanamke anaweza kuomba na kusifu katika kanisa, lakini mwanamke hawezi kuchunga na kusimamia kanisa la Mungu kwa kuwa mtume, mwalimu, askofu, mchungaji n.k, kwa sababu maandiko yanasema.

1 Timotheo 2:8 Basi, nataka WANAUME WASALISHE KILA MAHALI, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. 

Soma tena.

1 Timotheo 2:12 Simpi mwanamke RUHUSA YA KUFUNDISHA, WALA KUMTAWALA MWANAMUME, bali awe katika utulivu. 

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 

Na tena yanasema

1 Wakorinto 14:34  Wanawake na wanyamaze KATIKA KANISA, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 

35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. 

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? 

37 MTU AKIJIONA KUWA NI NABII AU MTU WA ROHONI, NA AYATAMBUE HAYO NINAYOWAANDIKIA, YA KWAMBA NI MAAGIZO YA BWANA.

38 LAKINI MTU AKIWA MJINGA, NA AWE MJINGA

Hivyo, andiko hilo la (Wafilipi 4:3) haliharalishi wanawake kuchunga makanisa, kusimama madhabahuni kusalisha, kuhubiri, na wala kufundisha katika katika makanisa, na kama wewe mwanamke unayesoma ujumbe huu ni miongoni  ni mwa hao wanaofanya haya au ni mchungaji mwanamke, askofu mwanamke, mtume mwanamke n.k, basi tambua kuwa, upo kinyume na neno la Mungu, (yaani ulidanganywa na kudanganyika), hivyo tubu na ukae katika nafasi yako kulingana na maandiko matakatifu.


Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)


Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 10)


Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?

8 thoughts on - Je! Andiko la (Wafilipi 4:3), linatoa ruhusa kwa wanawake kuchunga makanisa, kusimamia makanisa, na kusimama madhabahuni ili kuhubiri na kufundisha?
  1. biblia ina maana gani iliposema usitamani? at je! kunatofauti gani kati yakutamani kitu cha jerani yako na kupenda kitu ya jerani yako?

    1. Nilikukuwa nahitaji kulichukua hili somo ila sioni sehem ya kudownload,,,,
      Samahani msaada Kwa Hilo
      BWANA YESU ASIFIWE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *