USIWE WEWE MWENYE KUASI.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Ipo tabia nyingine ya Mungu tunayopaswa kuifahamu ambayo ni fundisho tosha kwetu sisi pindi tunaposoma wito wa Ezekieli kuhani, au nabii Ezekieli katika maandiko matakatifu.

Na tabia yenyewe si nyingine bali ni Mungu kumtaka mteule au muitwa, KUTO KUWA MUASI, (yaani kutokwenda tofauti na yale aliyoagizwa kuyafanya na kuyatenda, au mteule / Muitwa, kuto kusema chochote kile ambacho hajaangizwa kwa jina la Bwana). Ikiwa na maana kuwa, unaweza kweli ukaitwa na Mungu lakini bado ukawa muasi wa maagizo yake, unaweza kweli ukapokea neema ya wokovu kwa kuokolewa kutoka dhambini lakini bado ukawa muasi kama wale waliookolewa Misri walivyokuwa waasi. Ndio maana sasa, Mungu kwa kutaka kuonesha hilo, na kwamba hapendezwi na tabia hiyo, alimwambia nabii Ezekieli maneno haya.

Ezekieli 2:8 BALI WEWEMWANADAMUSIKIA NENO HILI NINALOKUAMBIAUSIWE WEWE MWENYE KUASI KAMA NYUMBA ILE YENYE KUASI; funua kinywa chako, ule nikupacho. 

Akimaanisha kuwa, tabia ya kuasi, au kutokufikisha ukweli wa Mungu kwa kuyapindisha na kuyageuza maagizo yake, au kutofanyia kazi maagizo ya Mungu ni jambo baya sana na lisilopendeza mbele za Mungu, kwani kwa kufanya hivyo, watu watazidi kuishi katika ukaidi wa maagizo ya Mungu daima (kuendelea kuwa waasi).

Mfano mzuri ni manabii na makuhani wa Israeli, ambao waliasi maagizo ya Mungu kwa kuyaharifu na kwa kutowafundisha watu sheria za Bwana (Ezekieli 22:26), na tena, kuwatabiria na kuwahubiria kwa jina la Bwana maneno ambayo Mungu hakuyaagiza, na hivyo kupeleka nyumba nzima ya Israeli kuwa waasi kama Bwana alivyowaita..

Ezekieli 44:6 Nawe UTAWAAMBIA WAASIYAANI NYUMBA YA ISRAELI, Bwana MUNGU asema hivi; Enyi nyumba ya Israeli, katika machukizo yenu yote, na iwatoshe, 

Ni nini Mungu anataka tujifunze?

Hata na wewe mkristo unayesoma ujumbe huu, uliyepata neema ya wokovu, uliyeitwa na Mungu kwenye utumishi wo wote ule, Mungu anakuasa katika huo utumishi wako na wito wako kuwa, USIWE MWENYE KUASI MAAGIZO YAKE, bali maneno yake yote uyapokee moyoni mwako na kuyasikia kwa masikio yako. Usiende kulia wala kushoto, usipunguze neno lake kwa sababu ya hisia zako na wala usiongeze neno kwa sababu ya maoni na mitazamo yako, simama katika neno lake tu basi, na wala usiachilie lolote lile kuanguka, (iga mfano wa Samweli).

1 Samueli 3:19 SAMWELI AKAKUA, naye Bwana alikuwa pamoja naye, WALA HAKULIACHA NENO LA LO LOTE LIANGUKE CHINI

Usiwe mwenye kuasi askofu kwa kupinga agizo la ubatizo, usiwe mwenye kuasi mchungaji kwa kupinga agizo la kushiriki meza ya Bwana, usiwe mwenye kuasi kwa kupinga agizo la Mwanamke kufunika kichwa awapo ibadani, usiasi na kupindisha maagizo ya Mungu kwa kusema Mungu ameruhusu kumwacha mke wako au mume wako, usiasi neno la Mungu kwa kuruhusu wanawake kuchunga na kusimamia makanisa (kuwa mitume, maaskofu, wachungaji n.k), usiasi maagizo ya Mungu kwa kuwafundisha wanawake kuvaa suruali na mavazi ya kikahaba na kiwafanya kuwa waasi, usiwe mwenye kuasi kwa kudanganya watu na kuwaambia Mungu amekuagiza uwauzie watu mafuta ya upako na maji ya upako, usiwe mwenye kuasi kwa kuwafariji watu katika dhambi zao na machukizo yao na kusingizia ni upendo wa Kristo, usiwe muasi kwa kuiasi injili ya Kristo, bali uyasikie na kuyatii maneno yote uliyoagizwa na Mungu (maandiko matakatifu)

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

 +255652274252/ +255789001312


LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, AU ATAKAYENENA KATIKA JINA LA MIUNGU MINGINE, NABII YULE ATAKUFA.Kwanini Gombo la chuo lililokunjuliwa mbele ya nabii Ezekiel likikuwa limejaa maombolezo, na vilio na Ole ndani yake? (Ezekieli 2:10).


MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.


Nini maana ya mstari huu “Nimesulubiwa pamoja na Kristo?” (Wagalatia 2:20)


Je! Ni watu gani hao wasamao Bwana, Bwana, lakini hawatoingia katika ufalme wa mbinguni? (Mathayo 7:21)

3 thoughts on - USIWE WEWE MWENYE KUASI.

  • biblia inasema katika meza ya bwana tunabidi tutumie mkate na divai, lakini kufatana na mazingira yahuku kwetu kupata divai ni shida sana tena inaomba garama kubwa kuipata hivo tumekuwa tukitumia jus badala ya divai, je! ni sahihi jambo hilo?

  • kuna mtumishi wa mungu hapa kijijini kwetu anatabiri, kuponya wagonjwa gafla, na kufunulia mtu, na anauwezo wakumwambia mtu hata majina ya ndugu zake, alifanya nini jana yaani kama nabii, lakini kilichonishangaza nikwamba akiona mtu na ugonjwa mkubwa anamwambia anunuwe mafuta yake 25$, je kwanamna hihi kweli anatumikisha uwezo wa roho mtakatifu?

LEAVE A COMMENT