Swali: kulingana na Yoeli 2:32 na Warumi 10:13 zinasema kuwa, kila atakayeliita jina la Bwana ataokoka, je! Jina hilo la Bwana ni Yesu Kristo?
Warumi 10:13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
Jibu: Ndio, jina hilo linalozungumziwa hapo ni YESU KRISTO kwani maandiko yanasema kuwa hakuna jina walilopewa wanadamu chini ya Mbingu litupasalo sisi kuokolewa kwalo
Matendo Ya Mitume 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Wakristo wengi kwa kukosa ufunuo wanashindwa kumwelewa Mungu na utendaji kazi wake na kuishia kuwa watu wa madhehebu kama mafarisayo. Utakuta mkristo wa leo anang’ang’ania kuwa jina la Bwana ni fulani na wala hataki kusikia neno lingine, sasa mtu kama huyo tayari amekosa Roho ya ufunuo, hivyo tunamuitaji sana Roho wa Bwana Yesu ili kutufunulia maandiko.
Sasa maandiko yanathibitisha kuwa jina la Bwana ni YESU KRISTO? Jibu ni ndio tusome
Yohana 5:43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
Bwana Yesu alisema kuwa, jina alilokuja nalo ni jina la Baba yake, hivyo basi kumbe jina ambalo yeye analo ni la Baba yake, kama yeye ni Yesu basi Baba yake naye ni Yesu Kristo na ndio maana nabii Yoeli alitabiri kuwa, kila atakayeliita jina la Bwana ataokoka akimaanisha jina hilo la Yesu Kristo.
Naandiko yanasema kuwa Bwana alijitambulisha kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama MUNGU MWENYEZI kwa Musa alijitambulisha kama Yehova (kutoka 6:3) Lakini Tomaso anamjua Bwana kama Yesu Kristo
Yohana 20:28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!
Na ndio maana sehemu nyingine anasema kuwa Heri kwetu sisi tutakaposhutumiwa kwa ajiri yake kwamaana ndivyo walivyowatenda manabii wote
Matayo 5:11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Umeona? Kumbe hata manabii waliokuwapo kabla yetu waliudhiwa kwaajiri ya Bwana Yesu.
Ndugu yangu ambaye unayemuona Bwana Yesu leo ni kama mtu wa kawaida tu! Fahamu kuwa ipo siku ambayo utapiga goti lako na kukiri kwa kinywa chako kuwa Yesu ni Bwana.
Isaya 45:23 Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Tena sehemu nyingine paulo anaurudia unabii huo wa Isaya kuwa kila ulimi utamkiri Mungu ambaye ni Bwana Yesu (Yohana 20:28)
Warumi 14:11 Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.
Hivyo ndugu yangu ni muda kusalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu na kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu kulingana na matendo 10:48 Matendo 19:5
Shalom.
Mada zinginezo:
Je! Hadi sasa kuna manabii wa Mungu?
Je! Ni kweli mshahara wa dhambi ni mauti na si moto wa milele?
Je! Ni lazima mgonjwa adongoke chini pale anapoombewa?
Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.