Nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo apewe sifa milele na milele amina. Ukisoma maandiko utagundua kuwa Bwana wetu na Mungu wetu Yesu Kristo alipanda mbegu zake njema hapa ulimwenguni ambazo ni wana wa ufalme.

Matayo 13:38  lile konde ni ulimwengu; ZILE MBEGU NJEMA NI WANA WA UFALME; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; 

Lakini katikati ya zile mbegu njema ibilisi nae alipanda magugu ambayo ni uzao wake, na hivyo Bwana akaruhusu yakue pamoja hadi wakati wa mavuno (Mathayo 13:30)

Sasa wakati yanakua pamoja ni wazi kuwa yalinyeshewa mvua moja ya Roho mtakatifu na kupata karama za Roho mtakatifu kama vile uponyaji, kunena kwa lugha n.k lakini siku zote wana wa ibilisi hawawezi kufanana na wana wa ufalme wa Mungu hata kama wana karama za Roho mtakatifu kwa maana wana wa ufalme ni zahiri na wa ibilisi pia kama maandiko yanavyosema katika.

1 Yohana 3:10  Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. 

Uzao wa ibilisi ndio unaotumia jina la Bwana Yesu huku wakifanya machukizo katikati ya kanisa, na haya machukizo yameongezeka sana wakati huu kuonesha kuwa ni wazi hizi ni siku za mwisho, utakuta watumishi wa Mungu wanafanya kampeni za kisiasa madhabahuni, wachungaji wanafanya uasherati na waumini wao, watumishi wa Mungu wanaoa wake zaidi ya mmoja, wanaacha wake zao na kuoa wengine, wanafungisha ndoa za jinsia moja Kanisani na wengine wakijiita ni maaskofu, wengine ni walevi katikati ya kanisa, Wengine ni wanzinzi katikati ya kanisa, haya yote ni machukizo mbele za Mungu na ibada zao ni HARUFU MBAYA mbele za Mungu kwani maandiko yanasema maombi ya watakatifu ni moshi wa manukato mbele zake (ufunuo 5:8) hivyo kama ni wanafanya machukizo ni wazi kuwa maombi yao ni harafu mbaya mbele za Mungu, jiulize unategemea Bwana atakufanya nini? 

Machukizo ni mengi sana katikati ya kanisa, utakuta kanisa lina mchungaji mwanamke na anasimama madhabahuni huku kavaa suruali, kavaa hereni na mamikufu, kajipodoa kwa makope ya bandia, makucha ya bandia, wanawake hawafuniki vichwa wakati wa ibada na wanasema kuwa wanamsufu Mungu. Ndugu yangu fahamu kuwa mnamtolea Bwana harufu  mbaya ya kunuka tu na Bwana atakuja kuyaondoa machukizo yote hayo na kuyatupa katika ziwa la moto 

Matayo 13:41  Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, 

Ndugu yangu ukijiona upo katika kanisa ambalo lina hayo machukizo toka hapo, kwani mmeshaanza kukusanywa kwenye matita matita kama unavyoona watu ambao mnafanana nao wa makanisa mengine wa aina yako nao walivyo makundi huko walivyokusanywa, ukijiona upo kwenye kanisa ambalo hukemewi uvaaji wako mbaya na hizo lipstick, na kucha za bandia, rasta, hereni, mawigi n.k toka huko kwani upo kati ya watu wachukizao na umeshaanza kukusanywa kwenye matitata.

Ndugu yangu, huu sio wakati wa kumtazama mtumishi fulani, sio muda wa kusema mbona mtumishi fulani mkubwa wa Mungu anavaa suruali, mbona mtumishi fulani mkubwa wa Mungu haongelei kitu hiki, mbona muhubiri fulani anafanya hivi,    Fahamu kuwa hao ni watumishi wa uongo, ndugu yangu ni muda wa wewe kutazama neno la Mungu linasema nini, ni muda wa wewe kukaa chini na kulisoma neno la Mungu kwa msaada wa Roho mtakatifu. Kumbuka kuwa huyo mtumishi wa Mungu unayemtazama na yeye pia atasimama mbele ya kiti cha enzi, hutohukumiwa kulingana na mawazo ya kiongozi wako wa dini bali kulingana na neno la Mungu tu.

Na ndio hao ambao watakuja kutimiza unabii wa Bwana Yesu 

Matayo 7:22  Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 

Hivyo kama upo katika hayo machukizo toka huko kwani huu ndio muda ambao wavunaji wameshatumwa kukusanya hayo magugu kwenye matita matika kama unavyoona sasa hivi, tafuta kanisa sahihi linalomwabudu Mungu katika Roho na Kweli

Bwana akubariki. Shalom 

KUFANYA MATENDO MEMA HAIMAANISHI KUWA UMESHAUPATA WOKOVU

Usimkatae (usimwache) Yesu aliye tumboni mwa Mariamu!

LEAVE A COMMENT