KWA MAANA ISRAELI AMETENDA KWA UKAIDI, KAMA NDAMA MKAIDI; SASA JE! BWANA ATAWALISHA KAMA MWANA KONDOO KATIKA MAHALI PENYE NAFASI?

Jina la Bwana na Mungu Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, karibu tujifunze maandiko. 

Biblia inasema katika.

Hosea 4:16 Kwa maana ISRAELI AMETENDA KWA UKAIDI, kama ndama mkaidi; SASA JE! BWANA ATAWALISHA KAMA MWANA-KONDOO KATIKA MAHALI PENYE NAFASI

Umeshawahi kujiuliza ni kwanini kanisa la sasa la Kristo halina Utukufu kama ule uliokuwapo katika kanisa la mwanzo? Hakuna tena imani kama ile iliyokuwapo mwanzo (bali ni unafiki na kuigiza), hakuna tena nguvu ya Mungu katika kanisa kama ile iliyokuwapo mwanzo, (na angali Mungu ni Yule Yule), hakuna tena ushukiwaji wa Roho Mtakatifu kwa watu katika kanisa kama mwanzo, hatuoni tena watu wakipokea Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa katika kanisa la mwanzo, hakuna tena ishara zinazofuatana na kanisa la Kristo ambazo Bwana Yesu (Asiyesema uongo), Alisema zitafuatana na hao waaminio (Marko 16:17-18). 


Je! Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini? 

Jibu ni kwamba, kanisa la Mungu, ambalo ndilo taifa la Israeli rohoni, LIMEFANYA UKAIDI, (kwa sababu taifa la Israeli la mwilini lilikuwa ni kivuli cha Kanisa la Mungu lijalo kule jangwani) 

Matendo Ya Mitume 7:37 Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye. 

38 Yeye ndiye aliyekuwa KATIKA KANISA JANGWANI pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. 

Na tena, hata sasa kanisa hili la Mungu ambalo ndilo taifa la Israeli rohoni, bado linaendelea kufanya ukaidi, kitu ambacho kinachompelekea Mungu kushindwa kulilisha chakula sahihi kama kile walicholishwa kanisa la kwanza, yaani nguvu ya Roho Mtakatifu katika kanisa, utukufu na kuangaza kwa kanisa katika giza, ishara, miujiza, karama n.k (kwa sababu ya ukaidi wao).

Hosea 4:16 Kwa maana ISRAELI AMETENDA KWA UKAIDI, kama ndama mkaidi; SASA JE! BWANA ATAWALISHA KAMA MWANA-KONDOO KATIKA MAHALI PENYE NAFASI

Kanisa limekuwa kaidi na ndio maana Bwana alilishi tena kama mwana kondoo alishwavyo au anavyolishwa katika malisho mazuri, (bali limekufa kwa ukame wa njaa kwa kukosa Nguvu ya Mungu)


Kanisa limekuwa kaidi kwa kutupilia mbali Injili iliyohubiriwa na mitume na manabii watakatifu.


Limekuwa kaidi kwa kutaka kuongozwa kwa mawazo yao na akili zao binafsi, limekuwa kaidi kwa kutaka kuongozwa na hisia zao na mitazamo yao binafsi, na sio tena sheria ya Kristo, limekuwa kaidi kwa kutaka kuongozwa na falsafa za wanadamu, theolojia za wanadamu, na wala si Maandiko Matakatifu tena, sasa je! Kwa hali hii ya ukaidi unaofanywa na kanisa kama vile ndama mkaidi, unategemea vipi Bwana kulilisha kanisa kama mwana-kondoo anavyolishwa mahali penye malisho mazuri? Jibu ni hapana.


Hivyo, ni lazima kanisa katika siku hizi za hatari kuacha ukaidi kwa kutupilia mbali hisia zao, mawazo yao, mitazamo yao, maoni yao na kulitii neno la Mungu (kuongozwa na maandiko matakatifu), ili Bwana aweze kulilisha Kanisa kama Mwana-Kondoo katika malisho mazuri.


Kumbuka: Bwana anakuja kwa ajili ya kile alichokiacha, yaani imani na Injili iliyohubiriwa na mitume na manabii wake watakatifu na wala sio kitu Kingine, hivyo jitahidi uingie sasa kwa nguvu kwa kuitii Injili ya Kristo.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe kanisa la Kristo ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

NAONA KUNA SINTOFAHAMU KUHUSU KRISMASI, HIVI NI KWELI IPO KWENYE MAANDIKO?


UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?



Nini maana ya mstari huu “na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorongwa vema” (Ezekieli 13:10)


FAHAMU NINI MAANA YA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24)

One Reply to “KWA MAANA ISRAELI AMETENDA KWA UKAIDI, KAMA NDAMA MKAIDI; SASA JE! BWANA ATAWALISHA KAMA MWANA KONDOO KATIKA MAHALI PENYE NAFASI?”
  1. AMEN, lakini nimesikia watu wengi wakisema hata watumishi ya kuwa pale mtu anapokufa uwaga anakutana na njia mbili, moja ya uzima, na ya motoni, akichagua ya mbinguni anaenda kwenye uzima wa milele, na akienda katika njia ya motoni anakumbana na mauti ya pili, swali: imani hihi ni yakweli? kama nihivo, kuna umuhimu gani wakuokoka basi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *