NAONA KUNA SINTOFAHAMU KUHUSU KRISMASI, HIVI NI KWELI IPO KWENYE MAANDIKO?

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

JIBU: Krismasi haipo sehemu yo yote ile katika maandiko matakatifu, na wala maandiko hayajasema popote pale kuwa Kristo alizaliwa Tarehe 25 December. 


Tofauti kabisa na sikukuu zingine kwenye maandiko kama vile, sikukuu za sabato, mikate isiyotiwa chachu, pasaka, pentekoste, sikukuu ya upatanisho, sikukuu ya vibanda, baragumu n.k, sikukuu ambazo zinafahamika miezi yake, na tarehe zake katika biblia (Walawi 23:1-43), na tena, maandiko yanatuambia kuwa, mtu yo yote yule asituhukumu kwa sikukuu hizo Yaani mikate isiyoltiwa chachu, pasaka, pentekoste, sabato n.k kwani zilikuwa zikimfunua Yesu Kristo.

Wakolosai 2:16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, AU KWA SABABU YA SIKUKUU AU MWANDAMO WA MWEZIAU SABATO

17 MAMBO HAYO NI KIVULI CHA MAMBO YAJAYOBALI MWILI NI WA KRISTO

Lakini Krismasi yenyewe haipo sehemu yo yote ile katika biblia takatifu, na zaidi sana Bwana Wetu Yesu Kristo alisema tumwamini Yeye KAMA VILE MAANDIKO YANAVYOSEMA (Yohana 7:38), na maandiko hayajasema Tarehe 25 ndio aliyozakiwa Yesu Kristo, hivyo basi, mtu yo yote yule anayesema Kristo alizaliwa tarehe 25 December ANASEMA UONGO JUU YA MWANA WA ADAMU kwani maandiko hayajasema hivyo. (Kwa hiyo ishia biblia ilipoishia).


Lakini je! Siku hiyo ya Tarehe 25 December sisi kama Wakristo hatutakiwi kufanya ibada? Jibu ni la! Siku hiyo unaweza mfanyia Mungu ibada kama zilivyo siku zingine tu, kuanzia asubuhi hadi jioni (kama utapendavyo), unaweza kwenda kuhubiri (kama utapenda), unaweza hata funga na kumwomba Mungu (kama utapenda), kwani maandiko yanasema inatupasa kumwomba Mungu siku zote (ikiwemo na hiyo Tarehe 25).

Luka 18:1 Akawaambia mfano, ya kwamba IMEWAPASA KUMWOMBA MUNGU SIKUZOTE, wala wasikate tamaa. 

Na tena, unaweza kuwaombea watu wengine katika siku hiyo kwani hata mtume Paulo alikuwa akiwaombea watu KILA SIKU (ikiwemo na siku hiyo ya Trh 25 ya mwisho wa Mwaka)


Licha ya hivyo, pia katika tarehe hiyo 25 December, unaweza pumzika kama ukipenda, unaweza Fanya shughuri zako za kila siku kama ukipenda, unaweza pika chakula kizuri na kula (kama utapenda), na unaweza lala na njaa au hata bila kula kabisa (kama utapenda), lakini hakuna uhusiano wote ule na kuzaliwa kwa Kristo, biblia haijasema Kristo kazaliwa Tarehe 25 December, hicho kitu hakipo kwenye maandiko.


Lakini wewe unayesoma ujumbe huu, ambaye umepanga Siku hiyo ya tarehe 25 kwenda kumtukuza na kumwabudu mungu wako (ibilisi), kwa kwenda kufanya uzinzi na mke wa mtu au mume wa mtu, kufanya uasherati na yule boyfriend au girlfriend wako, kwenda kulewa na wafanyakazi wenzako, kwenda night clubs na marafiki zako, kwenda kufanya fujo na uharifu n.k, umeshajiuliza swali hili kabla ya kuwaza hayo, je! itakuwaje saa ambayo wewe kijana upo juu ya huyo kahaba, au upo juu ya huyo boyfriend wako wewe binti, au upo juu ya huyo mke wa mtu wewe baba, harafu ndio saa ambayo unavuta pumzi yako ya mwisho na kukata roho hapo, umeshawahi jiuliza roho yako itaenda wapi ukifa katika hali hiyo? (Jibu unalo), sasa Kwanini usiache njia yako hiyo mbaya na mawazo yako hayo mabaya na umgeukia Mungu kama maandiko yanavyosema?

Isaya 55:7 Mtu mbaya na aache njia yake, NA MTU ASIYE HAKI NA AACHE MAWAZO YAKE; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. 

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

MMEKWISHA KUSHIBA, MMEKWISHA KUPATA UTAJIRI, MMEMILIKI PASIPO SISI.


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


“NA VITABU VIKAFUNGULIWA” NI VITABU GANI HIVYO? (Ufunuo 20:12).


UNAKO BISHA HODI NDIKO UTAKAKO FUNGULIWA, UNACHOKITAFUTA, NDICHO UTAKACHOKIONA


Tabia moja ya unafiki unayopaswa kuiepuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *