Yohana 17:16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
Bwana Yesu Kristo asifiwe.
Haya ni maneno ya Kristo Yesu, akiwatambulisha watu wanaomwubudu Mungu katika Roho na kweli (Wacha Mungu, watakatifu waliopo duniani)
Maswali ya kujiuliza ni je! ulimwengu ukoje
Mpaka Kristo aseme sisi si wa ulimwengu huu? Na je sisi ni wa wapi?
1 Yohana 2:15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Mambo yaliyoko duniani
1: Tamaa ya mwili
2: Tamaa ya macho
3: Kiburi cha uzima
Tamaa ya mwili ikoje?
Mapenzi, mavazi na mapambo ya kila namna, starehe, vyakula, vinywaji, fedha, maisha mazuri na fahari yote ya ulimwengu huu. Hivi ni vitu ambavyo kila mwenye mwili (binadamu) HUTAMANI maana viko duniani, lakini vitu hivi kwa wacha Mungu wa kweli kweli havitakiwi kuchukua nafasi kwenye mioyo yetu kwa maana vitu hivi ni vya muda tu. Tunatakiwa kuutumia ulimwengu kwa KIASI TENA KWA TAHADHARI KUBWA
Kristo anasema.
Yohana 17:15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
Soma tena
1 Wathesalonike 5:5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
Tukitembea kwa tahadhari na kwa kiasi “Tunalindwa” sasa wewe unayendelelea kukimbizana na namna ya ulimwengu huu, kila staili inayokuja duniani na wewe umo bila tahadhari, ndugu yangu Mungu hatakulinda na yule mwovu, na kwasababu hiyo kila aina ya roho chafu kutoka kwa yule mwovu zitapata nafasi ya kukaa kwako maana umebeba vitu vyao moyoni mwako. Neno linasema sisi si wa ulimwengu huu hapa tunapita tu.
1 Petro 2:11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Tamaa ya macho ikoje?
Macho ni kiungo kizuri sana na ni hatari sana, tumia macho yako vizuri, weka agano na macho yako kama Ayubu.
Ayubu 31:1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?
Macho ndiyo yanasababisha tamaa ya mwili kuwaka, maana macho yanatangulia kuona kila kitu, kiwe chema au kibaya na kupeleka taarifa kwenye moyo na akili yako na baada ya hapo inazaliwa TAMAA, na tunajua nini hutokea mwili ukishika nafasi yake ya utendaji. Ndipo utaelewa maana ya hili neno.
Yakobo 1:15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. ”
Kiburi cha uzima kikoje?
Kiburi cha Uzima ni kiburi mtu anachokipata kutokana na vitu alivyonavyo vya kidunia (hususani mali).
Watu ambao hawajamjua Mungu, uzima wao wameuweka kwenye mali, wanapokuwa na mali nyingi ndipo wanapojiona wao ni watu (wenye uzima), wakikosa wanajiona wao si kitu.. hivyo inapotokea wanapata mali hizo, zinawapa kiburi na kuwafanya wabadilike tabia mbele za Mungu na wanadamu.
Lakini Bwana Yesu alisema maneno haya..
Luka 12:15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
Sisi ni wa wapi?
Yohana 15:18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
Tunasoma tena katika
1 Wakorintho 15:47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.
48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
Mwisho nimalizie kwakusema tusiipende dunia na mambo yake kwakua dunia na mambo yake itapita, Bali Neno la Mungu halitapita kamwe. Kama hujampa Kristo maisha amua Leo kwa maana SAA YA WOKOVU NI SASA.
Umebarikiwa na Kristo.
Mada zinginezo:
KUFANYA MATENDO MEMA HAIMAANISHI KUWA UMESHAUPATA WOKOVU
“Mke wa ujana wako” anayezungumziwa katika biblia ni yupi?
Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.
USIBATILISHE KAZI YA MSALABA WA YESU KWA INJILI ISIYOWEZA KUOKOA ROHO ZA WATU.
Amen, barikiwa sana
Amen, nawe pia mpendwa.