Nini maana ya mstari huu “Nimesulubiwa pamoja na Kristo?” (Wagalatia 2:20)

SWALI: Nini maana ya Nimesulubiwa pamoja na Kristo kama mtume Paulo alivyosema katika (Wagalatia 2:20)?

Wagalatia 2:20 NIMESULUBIWA PAMOJA NA KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. 

JIBU: Ili tuweze kuelewa maana ya “kusulubiwa pamoja na Kristo”, hatuna budi kwanza kufahamu Kristo alisulubiwa vipi kwa kuchunguza jinsi alivyosulubiwa, na ndipo tutakapokuja kuelewa maana ya maneno hayo. 


Tukisoma maandiko yanatuambia kuwa, Kristo alisulubiwa kwa kutundikwa juu mti, (uwe wa msalaba au vyovyote vile), lakini maandiko yanasema alisulubiwa juu mti sawasawa na maandiko ya torati ambayo  aliyokuja kuyatizima.

Kumbukumbu La Torati 21:22 Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa,  NAWE UKAMTUNDIKA JUU YA MTI; 

23 MZOGA WAKE USIKAE USIKU KUCHA JUU YA MTI; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako. 

Sasa ukichunguza kwa makini jinsi mtu anavyotundikwa au kusulubiwa mtini, utagundua kuwa, mtu huyo anakuwa hawezi tena kusogeza mikono yake wala miguu yake kama mwanzo, yote inabaki pale pale, na pia katika utundikwaji au usulubishwaji wake ni lazima itumike misumari ya kumkazia pale mtini, na pia ni lazima kuwe na nyundo ya kupigilia misumari na kumkaza yule mtu mtini kiasi kwamba, anakuwa hawezi tena kusogeza miguu yake na mikono yake popote pale kama mwanzo.


Hivyo ndivyo inavyokuwa rohoni kwa mtu yule aliyesulubiwa pamoja na Kristo, anapigiliwa na kukazwa kwa misumari (Isaya 22:23), na kugongelewa kwa nyundo ambayo ni neno la Mungu kiasi kwamba mtu huyo anakuwa hawezi tena kusogeza mikono yake na kwenda kuiba tena au kupokea rushwa tena kama mwanzo, anakuwa hawezi tena kusogeza mikono yake na kushika pombe na sigara na kuanza kulewa au kuvuta kama mwanzo, hali kadhalika na miguu pia, inapigiliwa kwa neno la Mungu ambalo ni nyundo kiasi kwamba inakuwa haiwezi tena kusogea na kwenda sehemu za mchukizo kama mwanzo, kwanini? kwa sababu anakuwa amesulubiwa na kupingiliwa misumari kwa neno la Mungu ambalo ni nyundo, na kukaa hapo kwa kushikiriwa na neno, yaani kukaa katika neno tu si huko na huko kama hapo kwanza (huko ndiko kuendenda katika upya).


Hivyo basi, kama wewe ni mkristo lakini miguu yako kutwa kukimbilia kwenye mikesha ya anasa na ya kudunia, miguu yako kutwa kukimbilia kwenye night clubs na vijiwe vya mipira na kubeti, kutwa inakimbilia huko na huko kwenda kufanya uzinzi na uasherati, kwenda kufanya uuaji na ubakaji, inakimbilia huko na huko kwenda kwa waganga, kwenda kuabudu sanamu na kuwaomba wafu, kutwa kwenda kukimbilia mafuta ya upako na maji ya upako, basi tambua kuwa hujasulubiwa pamoja na Kristo, hivyo miguu yako na mikono yako inahitaji kupigiliwa misumari ya Mungu (Isaya 22:23) na kukogongelewa kwa nyundo ambayo ni neno la Mungu (Yeremia 23:29), ili ubaki hapo katika neno na usiende tena huko.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Bwana wa mavuno ni nani? (Mathayo 9:38)


Kwanini mfalme Hezekia aliiita kwa jina “Nehushtani” ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa kule jangwani?


Kwanini safari ya wana wa Israeli kuelekea nchi yao ya ahadi (kaanani) ilikuwa imeshamiri vita?


MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.

One Reply to “Nini maana ya mstari huu “Nimesulubiwa pamoja na Kristo?” (Wagalatia 2:20)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *