Je! Agizo la Bwana kwa mitume wake la kufufua wafu lilikuwa ni kwa baadhi ya mitume tu?


Matayo 10:5 HAO THENASHARA YESU ALIWATUMA, AKIWAAGIZA, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.

 6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

 7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.

 8 Pozeni wagonjwa, FUFUENI WAFU, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 

SWALI: Je! Agizo hilo la Bwana kwa mitume wake la kuwafufua wafu lilikuwa ni kwa baadhi ya mitume tu na si wote? Kwa sababu tunaona katika maandiko matakatifu kuwa, hakuna sehemu yoyote ile iliyorekodiwa mtume Yohana akifufua wafu, wala mtume Yakobo, wala mtume Mathayo mtoza ushuru, wala mtume Thadayo, isipokuwa Petro tu kati ya wale thenashara na mtume Paulo ambaye alitokea baadae baada ya Bwana kupaa.


JIBU: Agizo hilo la Bwana la kufufua wafu halikuwa kwa baadhi ya mitume tu, la hasha! Kwa sababu kama ingekuwa hivyo ni wazi kuwa, Bwana angesema Petro kafufue wafu na ninyi wengine mkafanye hichi au kile, lakini badala yake tunaona hakusema hivyo, bali alitoa agizo hilo kwa wote kwa kusema..

Matayo 10:8 Pozeni wagonjwa, FUFUENI WAFU, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 

Ikimaanisha kwamba, agizo hilo ni kwa wote. Lakini pia, tukisoma maandiko hatuoni sehemu yoyote ile iliyorekodiwa hao Thenashara wakifufua wafu isipokuwa Petro tu peke yake, na tena Petro mwenyewe alimfufua mfu mmoja tu Tabitha (Dorkasi). Umeona hapo?…

Sasa pasipo kumruhusu Roho Mtakatifu kutufundisha alimaanisha nini hapo, au kuna aina gani nyingine ya wafu, tutaishia kuona biblia ina mapungufu na inajichanganya tu, kwa sababu huku anasema mkafufue wafu, lakini huku hatuoni hao mitume wenyewe wakifanya hivyo, na wale waliofanya hivyo hawakufufua wafu zaidi hata ya watano, kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. 


Mitume wa Bwana walifufua wafu wengi sana tofauti na sisi tunavyodhani, mitume walifufua wakuu wa masinagogi, mafarisayo na masadukayo, maakida na maaskari, maliwali wenye akili na wanawake wenye vyeo, maskini, wachawi, n.k, hawa wote ni baadhi tu ya wafu ambao mitume waliwafufua. Sasa unaweza uliza kivipi?…Jibu ni kuwa, ipo aina nyingine ya wafu katika biblia tofauti na ile tunayoidhania kila siku.

Biblia inasema katika…

Waefeso 2:1 Nanyi MLIKUWA WAFU KWA SABABU YA MAKOSA NA DHAMBI ZENU;

Kumaanisha kuwa, watu wowote wale wanaoishi katika dhambi (wasio mwanimi Yesu Kristo) ni WAFU PIA.

Umeona hapo aina nyingine ya wafu katika biblia?..Na aina hii ya wafu ndio ambayo ilifufuliwa kwa wingi mno na mitume (Ndio maana aina ile ya kwanza ya wafu unaona ni wachache sana waliofufuliwa na mitume, na tena si zaidi hata ya watu wawili). Hivyo, mitume wengine walifufua wafu? Jibu ni ndio. Wafu gani?..wote waliokuwa katika dhambi (waliokuwa hawajamwamini Yesu Kristo, hao pia ni wafu ambao mitume waliwafufua). 


Lakini hata sasa pia, Yesu Kristo Mtume Mkuu (Waebrania 3:1), bado anaendelea kutoa agizo hilo hilo na si kwa mitume tu, bali kwa kila mkristo mwenye kuijua kweli duniani, kwenda KUFUFUA WAFU katika siku hizi za mwisho, katika siku ambazo wengi  wamekuwa wafu kutokana na kuishi katika dhambi kunakosababishwa na mafundisho na makanisa potofu na ya uongo duniani, anakuagiza wewe unayesoma ujumbe huu kuwa, nenda ukafufue wafu kwa kuwahubiria habari njema ya msamaha wa dhambi unaopatika kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika maji tele na jina lake sawasawa na (matendo 2:38)


Umepewa neema ya wokovu bure, kafufue wafu kwa kumuhubiri Yesu Kristo bure.


Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.


FUNZO KATIKA HABARI YA DANIELI NA MAANDISHI YALIYOANDIKWA NA VIDOLE VYA MWANADAMU KATIKA UKUTA WA ENZI YA MFALME


NAO WATAJIEPUSHA WASISIKIE YALIYO KWELI


ONYO..!! EPUKA KUTOA MANENO YA UONGO KATIKA SALA ZAKO.



MMEKWISHA KUSHIBA, MMEKWISHA KUPATA UTAJIRI, MMEMILIKI PASIPO SISI.


UNAKO BISHA HODI NDIKO UTAKAKO FUNGULIWA, UNACHOKITAFUTA, NDICHO UTAKACHOKIONA

2 thoughts on - Je! Agizo la Bwana kwa mitume wake la kufufua wafu lilikuwa ni kwa baadhi ya mitume tu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *