Je! Jina la mtume Yuda Iskariote ni miongoni mwa yale kumi na 12 yaliyoandikwa katika misingi kumi na miwili ya mji mtakatifu?

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Swali: Samahani naomba kuuliza, Je! Jina la mtume Yuda Iskariote ni miongoni mwa majina yaliyoandikwa kwenye misingi kumi na mbili ya mji mtakatifu? kwa sababu biblia inasema Yuda Iskariote alimsaliti Bwana Yesu. Na je! Majina ya mitume kumi na wawili yaliyoandikwa kwenye misingi hiyo kumi na miwili ni yapi?

Ufunuo 21:14 Na ukuta wa mji ulikuwa na MISINGI KUMI NA MIWILI, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya WALE MITUME KUMI NA WAWILI  wa Mwana-Kondoo. 

JIBU: Kitendo cha Yuda Iskariote kumsaliti Bwana Yesu hakibatilishi ukweli kwamba, alikuwa ni miongoni mwa mitume wa Bwana wakati akiwa hapa duniani katika mwili wa damu na nyama, hapana! Hiyo haibadilishi ukweli huo hata kidogo, ukweli unabaki vile vile kuwa, Mwana-Kondoo alipokuwa duniani kabla ya kuchinjwa, alikuwa na mitume kumi na wawili tu! Na si zaidi, na Yuda Iskariote akiwa miongoni mwao.

Lakini kabala ya kufahamu kama jina la Yuda Iskariote lilikuwepo au la! Na majina hayo ya mitume kumi na mawili ni yapi, ni muhimu kwanza tuelewe kwanini mji huo misingi ya kuta zake iwe na majina ya mitume kumi na wawili. Sasa Ili tuelewe hilo vizuri, tusome kifungu kifuatacho katika kitabu hicho hicho cha ufunuo…

Ufunuo 21:2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, KAMA BIBI-ARUSI ALIYEKWISHA KUPAMBWA KWA MUMEWE

Umeona hapo? mji huo ambao mtume Yohana aliuona ukishuka kutoka mbinguni unafananishwa na bibi arusi ambaye ni kanisa, aliyekwisha kupambwa tayari kwa mumewe yaani Yesu Kristo. Hiyo ni kumaanisha kuwa, mji huo unawahusu watu watakatifu tu! ambao ni bikira safi kwa mumewe ambaye ni Kristo, na ndilo kanisa ambalo litakalo nyakuliwa na kwenda kumlaki Bwana hewani siku ile (1 Wathesalonike 4:16-17), 

Hivyo, ukuta wa mji huo kujengwa juu ya misingi kumi na miwili yenye majina kumi na mawili ya mitume, inamamaanisha kwamba, watakatifu wa Yesu Kristo au kanisa la Kristo ambalo ni bibi arusi, limejengwa juu ya mafundisho ya Yesu Kristo ambayo yalikabiziwa kwanza kwa hao mitume kumi na wawili aliowachagua yeye mwenyewe kabla ya kuchinjwa, (Kama dhehebu lako, taasisi yako na shirika lako la kidini limejengwa juu ya mapokeo ya mababu, au mawazo ya msomi na professa faulani mwenye PHD ya biblia, au mawazo ya askofu wako, au papa wako, au padri wako, au mchungaji wako, tambua kuwa huna sehemu katika huo mji),

Na wakati huo ambao mwana kondoo alipokuwa duniani hakukuwa na mtume mwengine yoyote yule zaidi ya hao kumi na wawili hadi alipochukuliwa juu katika Utukufu, hao ndio mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo, waliokula nae, kulala nae na kunywa nae, ambao mtume Yohana anasema…

“na katika ile misingi majina kumi na mawili ya WALE MITUME KUMI NA WAWILI  WA MWANA-KONDOO”

Hapo hausiki mtume Barnaba wala Paulo kwa sababu wao walikuwa mitume baada ya Mwana kondoo kuchinjwa na kuchukuliwa juu, wala hausiki mtume Mathiya kwa sababu yeye alikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa Yesu Kristo wakati mitume kumi na wawili wa Mwana kondoo walipokuwa duniani na Mwana-Kondoo, wala hausiki mtume Yakobo mdogo wake Bwana Yesu (Wagalatia 1:19), na wala hawahusiki mitume wengine wowote wa Bwana ambao wapo leo hii na watakaokuja.

Sasa utauliza, inakuwaje? Mbona Yuda Iskariote alimsaliti Bwana Yesu harafu awe mbinguni? Jibu ni kwamba, mtume Yohana hakusema kama mtume Yuda Isakarote alikuwepo pale, wala hakusema mtume Andrea alikuwepo pale, wala Petro, wala Tomaso, wala Mathayo, bali alisema MAJINA YAO ndiyo yaliyoandikwa pale, likiwemo na lake mwenyewe mtume Yohana aliyeyaona maono hayo, ni kama vile tu majina ya kabila kumi na mbili za Israeli yalivyoandikwa kwenye milango ya mji huo, na ndivyo majina kumi na mbili ya mitume wa Mwana-kondoo yaliyoandikwa kwenye misingi kumi na mbili ya mji huo ambayo ni…

Matayo 10:2 NA MAJINA YA HAO MITUME KUMI NA WAWILI NI HAYA; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 

3 Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo; 

4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti. 

Je! Umeshampa Bwana maisha yako? Je! Unafahamu kuwa Bwana anakuja kuwachukua watu wake siku yoyote na saa yoyote ile? Na pia unatambua kuwa, hata kama hatorudi leo wala kesho lakini huna mapatano na kifo na endapo ukifa utaacha vyote na hukumu inafuata? Je! unatambua Kama pesa zako benki, cheo chako, wadhifa wako, umaarufu wako, kazi yako, mama yako, baba yako, mjomba wako, na watoto wako, hawawezi kukusaidia siku ya kifo chako? Hivyo fanya uamuzi sahihi leo wa kukimbilia kwa Yesu Kristo kwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa JINA LA YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako na utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu 

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Ni Mtume gani aliyekuwa Mkuu na Wa kwanza  kuliko wote katika biblia?


Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)


Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?


 Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?


Jifunze tabia hii kutoka kwa mtume Paulo.


JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA MITUME ANDREA NA FILIPO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *