Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?

JIBU: Shalom, tusome kwanza huo mstari.

1 Wakorinto 11:5  Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. 

Wakristo baadhi siku hizi wanatumia huu mstari kuhalalisha wanawake kusimama madhabahuni na kufundisha, pale maandiko yanaposema “mwanamke asalipo au anapohutubu” na hivyo husema kuwa, hata wanawake wanayo ruhusa ya kuhutubu na kufundisha madhabahuni kwani biblia imehalarisha hilo jambo, lakini swali ni je! Kweli andiko hilo linamaanisha hivyo? Jibu ni la! Kuhutubu kunapozungumziwa hapo katika 1 wakorintho 11:5 sio kuhubiri wala kufundisha bali ni kutoa unabii, kwa lugha ya kiingereza “to prophesy” hivyo basi kuhutubu  kunapozungumziwa hapo sio kuhubiri madhabahuni bali ni kutoa unabii.

Nje ya kanisa, mwanamke anaweza kutoka na kwenda kushuhudia watu habari njema za ufalme wa Mungu, anaweza kwenda kufanya uinjiristi kwa majirani zake, Kazini kwake, kwa ndugu zake, na hata kufundisha huko. Anaweza kwenda hata kwa watu mbali mbali na kuwaombea huko na kutoa mapepo kama amearikwa na watu kwa kadiri Roho wa Bwana atakavyomtumia. Lakini anapokuja kanisani, sehemu ambayo wanaume na wanawake wamekusanyika hana ruhusa ya kusimama madhabahuni kuhubiri au kufundisha 

Neno la Mungu linasema hivi katika 

1 Wakorinto 14:34  Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 

35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. 

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? 

37 MTU AKIJIONA KUWA NI NABII AU MTU WA ROHONI, NA AYATAMBUE HAYO NINAYOWAANDIKIA, YA KWAMBA NI MAAGIZO YA BWANA.

38 Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga. 

Wewe mwanamke unayejiita askofu/mchungaji litambue hilo agizo la Bwana, huna ruhusa kusimama madhabahuni na kufundisha lakini kama ukitaka kuwa mjinga endelea kuwa mjinga, ndivyo maandiko yanavyosema.

Haijalishi umemuona Bwana Yesu mara ngapi au amekutokea mara ngapi, wito wake hauwezi zidi neno lake. Hivyo acha kusimama hapo madhabahuni katika kanisa na kufundisha mwanamke.

Bwana akubariki. Shalom 


Mada zinginezo:

Mariamu Magdalene alikuwa ni mtume? (Yohana 20:17) 

 

Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?


Je! Ni kweli mtume Paulo alipingana na maandiko ya nabii Yoeli? (Yoeli 2:28)


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


KANISA LA KWELI NI LIPI DUNIANI?

2 thoughts on - Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *