Kwanini Kuzimu kuongeze tamaa yake na kufunua kinywa chake bila kiasi? (Isaya 5:14).

Kuzimu, Uncategorized No Comments

SWALI: Naomba kuuliza, hivi ni kwanini tukisoma maandiko yanasema kuzimu kumeongeza tamaa yake (ukubwa wake), na kufunua kinywa chake BILA KIASI?

Isaya 5:14 KWA HIYO KUZIMU KUMEONGEZA TAMAA YAKEKUMEFUNUA KINYWA CHAKE BILA KIASI; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. 

JIBU: Ni kweli kabisa kuwa, ipo sababu ya kwanini maandiko yaseme kuzimu kumeongeza tamaa yake (ukubwa wake) kwa sababu kinyume chake tukisoma Maandiko hatuoni yakisema pia mji ule Mtakatifu (Yerusalemu mpya) na wenyewe ukiongeza tamaa yake (ukubwa wake), na kufunua kinywa chake bila kiasi bali vipimo vyake vipo vilele.

Ufunuo 21:15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 

16 NA ULE MJI NI WA MRABANA MAREFU YAKE SAWASAWA NA MAPANA YAKE. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. 

Swali ni kwanini?

Hii ni kutupa picha harisi ya idadi ya watu ambao hawataki kumtii Mungu leo hii (injili Yake), kuwa ni wengi mno kipita kiasi na maelezo, na ndio maana kwa kujua hilo, Roho wa Yesu Kristo kupitia kinywa cha nabii Isaya alisema kuzimu imeongeza ukubwa wa kinywa chake kupita kiasi, kumaanisha watu wanao shuka huko ni wengi mno (wanaokufa pasipo kuitii injili ya kweli ya Mungu iliyohubiriwa na watumishi wake waaminifu). La sivyo kusingekuwa na umuhimu wo wote ule wa kufunua kinywa chake bila kiasi, lakini hadi inafunua kinywa chake BILA KIASI maana yake ni kuwa, wanaoenda huko nao ni WENGI BILA KIASI. 

Na mfano wa watu hao wengi kupita kiasi, ni watu wa dunia ile ya wakati wa Nuhu, ambapo watu wote duniani (isipokuwa watu nane tu) waliangamia na shuka huko kuzimuni kwenye vifungo.

1 Petro 3:19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 

20 WATU WASIOTII HAPO ZAMANI, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 

Na wengine ni wale watu wa Sodoma, Gomora na miji ya kando kando.

Yuda 1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, WAKIADHIBIWA KATIKA MOTO WA MILELE

Na ndio maana Bwana Yesu alipoulizwa kama je! Wanaookolewa ni wachache? Jibu la Bwana lilikuwa ni hili.

Luka 13:23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 

Hivyo mpendwa, katika dunia hii ya sasa tunayoishi, usithubutu kuishi kwa kutazama watu wengi wanafanya nini, usithubutu kuishi kwa kusema, mbona wanawake wengi tu na sehemu mbali mbali wanavaa vimini na suruali, mbona watu wengi tu wanaishi pamoja na kufanya tendo la ndoa na huku hawajafunga ndoa, mbona makanisa mengi tu yanabatiza watoto wachanga, mbona makanisa mengi tu yanabatizwa kwa jina la Baba, na Mwana, Na Roho Mtakatifu, mbona watu wengi tu karibia duniani kote wanazisijudia sanamu za Mariamu, za Yesu na za masanamu ya ng’ombe, mbona watu wengi tu wanatumia mafuta ya upako, mbona watumishi wa Mungu wakubwa wengi wanafanya hivi na vile, mbona Makanisa Mengi tu yanaruhusu wachungaji na maaskofu wanawake n.k, ndugu mpendwa, tambua kuwa Mungu hana wengi wape, vinginevyo angeangamia Nuhu na familia yake na ulimwengu mzima kuwa hai, au angeangamia Lutu na wanawe tu na watu wote wa Sodoma na Gomora wangekuwa hai (lakini sivyo).


kuzimu kumeongeza tamaa yake, na kufunua kinywa chake bila kiasi, kumaanisha wasiomtii Mungu (injili Yake iliyohubiriwa na mitume na manabii wake na watakatifu ni wengi mno), akiwemo na huyo kiongozi wako wa dini anayekufundisha mambo yaliyokinyume kinyume na maandiko matakatifu.

Tafadhari washirikishe na wengine wa ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


MADA ZINGINEZO:

LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, AU ATAKAYENENA KATIKA JINA LA MIUNGU MINGINE, NABII YULE ATAKUFA.


MAOMBOLEZO YA ROHO KWA KANISA.


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 10)


Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.


Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *