MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 05)

Siku za Mwisho, Uncategorized No Comments

Bwana Yesu apewe sifa. Nakukaribisha tena katika mfululizo wa makala hii inayoangazia makanisa na mafundisho ya uongo yanayopotosha watu wengi nyakati hizi za mwisho, kama hukufanikiwa kupata makala za nyuma zilizopita, basi, unaweza tuma ujumbe kwenda namba +255755251999 au +255625574252  au waweza tembelea website yetu ya www.rejeabiblia.com ili kupata mfululizo wa makala hizo zilizopita.

Hii ni sehemu ya tano (05) ya mfululizo wa makala yetu, karibu.


MAKANISA YA WAALIMU NA WAHUBIRI WA INJILI ZA MAFANIKIO 

Moja ya makanisa na mafundisho unayopaswa kuyakimbia ni haya, kwa sababu mahubiri na mafundisho hayo ya waalimu na wahubiri wanaokwambia njoo ufunguliwe kiuchuni, njoo upate kazi, njoo upate nyumba, gari, mke, mume n.k, au njoo ununue mafuta ya pako na ya kinabii, au chumvi ya upako, vitambaa na maji ya upako, sio tu kwamba ni ya uongo, hapana! bali ni ADUI WA MSALABA WA YESU KRISTO, watu ambao akili zao na mawazo yao ni ya vitu vya dunia hii tu!….watu hawa biblia inatuonya tukae nao mbali kwa usalama wa nafsi zetu

Wafilipi 3:18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, NA SASA NAWAAMBIA HATA KWA MACHOZI, KUWA NI ADUI ZA MSALABA WA KRISTO; 

19 MWISHO WAO NI UHARIBIFU, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, WANIAO MAMBO YA DUNIANI. 

Ndugu unayekimbilia kwa waalimu na wahubiri hao wa injili za mafanikio ambao ni adui za msalaba wa Yesu Kristo, hebu jiulize swali hili, je! Ni kweli kabisa Mungu anataka mimi nifunguliwe kiuchumi wakati bado ninaishi na mume au mke wa mtu? Au ni kweli kabisa Mungu anataka mimi nifundishwe na kuhubiriwa jinsi gani ya kupata magari na majumba pekee katika dunia hii ambayo Mungu ataiangamiza Yeye Mwenyewe kwa moto? 

Sefania 3:8 Basi ningojeni, asema Bwana, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; KWA MAANA DUNIA YOTE ITATEKETEZWA KWA MOTO WA WIVU WANGU.  

Au Mungu hataki kabisa ufundishwe na kuhubiriwa juu ya vitu vizuri alivyoviandaa katika mbingu mpya na nchi mpya kwa ajili ya watakatifu wake? 

1 Wakorinto 2:9 lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 

Mpendwa tambua hili, mitume na manabii wa Yesu Kristo hakufundisha wala kuhubiri injili ya mafanikio unayoisikia leo hii kwa hao watumishi wa uongo, wala Bwana Mwenyewe, bali alihubiri watu kutubu dhambi zao kwa kumwamini yeye na kubatizwa, na endapo tusipotaka kufanya hivyo tutapata hasara ya nafsi zetu na kuhukumiwa milele, hivyo, ukiona unafundishwa na kuhubiriwa injili yoyote ya njoo upokee maji ya upako, ufunguliwe kiuchumi, njoo upokee majumba na magari, injili ambayo kitovu chake sio cha kujikana nafsi yako na kujitwika msalaba wako na kumfuata Kristo, basi, tambua kuwa upo chini ya mtumishi wa shetani.


Kimbia huko kwa sababu idadi yenu kubwa ninyi wafuasi mnaowafuata hao waalimu na wahubiri wa injili ya mafanikio, inafunua kuwa mmekusanywa katika matita matita (jinsi mlivyo wengi), na mnakusanywa katika hayo matita matita kutokana na kukataa kwenu kutupa chini mizigo ya dhambi kama vile kuacha mapambo na fashion, kuacha kuvaa nusu uchi, vimini na suruali kwa wanawake, kuacha ulevi na uzinzi, kuacha miziki ya kidunia na anasa za ulimwengu huu, utoaji mimba, usengenyaji, huyo mume wa mtu umayeishi nae, ufisadi, na umwagaji damu zisizo na hatia na huku unapenda mafanikio, hivyo, kutokana na dhambi usizotaka kuziacha na harafu unataka mafanikio, mnakusanywa katika hayo matita matita na kupotezwa milele.

Matayo 13:30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, YAKUSANYENI KWANZA MAGUGU, MYAFUNGE MATITA MATITA MKAYACHOME; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. 


Toka huko sasa unusuru nafsi yako kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa katika maji tele na kwa JINA LA YESU KRISTO ili upate msamaha wa dhambi zako.

Hizi ni siku za mwisho, usikubali kupotezwa na makanisa na mafundisho ya uongo;

Shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Unasema Kwa lugha mpya?


Ni maovu yapi yanayotoka kinywani mwa Bwana kulingana na (Maombolezo 3:38)


AKAJIBU AKASEMA, NAENDA, BWANA; ASIENDE.


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 01)


UNAKO BISHA HODI NDIKO UTAKAKO FUNGULIWA, UNACHOKITAFUTA, NDICHO UTAKACHOKIONA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *