MALEZI YA WATOTO (SEHEMU YA KWANZA) 

Uncategorized, Watoto No Comments

FUNDISHO MAALUMU KWA MZAZI / MLEZI.

Katika vitu ambavyo ni vya muhimu na vya kuzingatia kwa wazazi au walezi, ni  uangalizi wa hali ya juu wa watoto tangu udogo wao, kwa sababu, ukisha haribu misingi ya malezi ya mtoto tokea akiwa mdogo, pindi atakapo kuja kuwa kijana au mtu mzima, anakua ni mzigo na mwiba katika jamii, Taifa kwa ujumla, na kwa mama yake.

Mithali 10:1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;  BALI MWANA MPUMBAVU NI MZIGO WA MAMAYE.

Sasa wewe kama mzazi au mlezi, unapaswa kufahamu kuwa, jawabu letu katika malezi ya watoto si lingine, bali ni Bwana Wetu Yesu Kristo, kwa kumruhusu kuwa Mwanzo wa kila hatua katika malezi ya watoto, kwa sababu Yeye Mwenyewe Alisema katika..

Mathayo 19:14 Lakini Yesu akasema, WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGUWALA MSIWAZUIE; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.

Lakini leo, tutajifunza malezi ya mtoto  aliye na umri wa kuanzia mwaka 0 hadi miaka mitatu (03).

Kwanza kabisa, Jambo la kwanza kwa wewe mzazi au mlezi, unatakiwa uwe ndani ya Kristo, yaani umeshatubu dhambi zako kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, na kupokea Roho Mtakatifu ambaye ni muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30). Na ukisha kizi hivyo vigezo, basi yafuatayo ni ya kuzingatia juu ya mtoto wako.

  1. Mweke mtoto wako wakfu mbele za Bwana madhabahuni kanisani

kumuweka wakfu mtoto madhabahuni kanisani ni kumbariki mtoto na kufungua njia ya kumwamini Mungu tangu akiwa na mwaka sifuri au zaidi, na  hii itampa mtoto nafasi ya Mungu kutembea nae katika udogo huo huo, na pia, hapa pana uhitaji wa kuelewa vizuri zaidi tunapo sema, “kumweka mtoto wakfu”..haina maana kuwa mtoto anaupokea wokovu bali maana yake ni kwamba, kumwekea ulinzi wa ki-Mungu katika ukuaji wake na Baraka kutoka kwa Bwana.

Marko 10:16 AKAWAKUMBATIAAKAWEKA MIKONO YAKE JUU YAOAKAWABARIKIA.

2. Kumwombea mtoto na kwenda nae nae ibadani 

Licha ya kumweka wakfu kwa Bwana, unapaswa pia kuwaombea watoto wako mbele la Bwana kila mara unapokuwa katika Kuomba, waombee watoto wako mema mbele za Bwana kama vile mama yao mtume Yakobo na Yohana alivyofanya.

Mbali na hilo, jambo lingine ni kwenda na mtoto ibadani, kwasababu, katika ibada pia, malaika wa Bwana hujiudhulisha kwa wingi sana kwa lengo la kuwahudumia watakatifu, hivyo wanaposhuka kwa lengo hilo mtoto nae atakuwa ni sehemu ya hao watakao hudumiwa.

Waebrania 1:13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

3. Mwimbie nyimbo za Injili, sifa, kuabudu na tenzi za rohoni

Katika vitu vya msingi na vya kuzingatia pia ni hapa, kwasababu maneno ni roho, hivyo, kamwe mzazi usiruhusu kumfundisha na kumzoesha mwanao kusikiliza miziki ya kidunia, au mtu awe anamwimbia miziki ya kidunia iliyojaa uzinzi ndani yake na matusi ya namna mbali mbali, kwani kwa kufanya hivyo, utakuwa unapanda mbegu ya shetani ndani yake, bali mwimbie nyimbo za injili, sifa, au tenzi za rohoni ili kumfanya akili yake imjue Mungu zaidi kuliko vitu vingine katika hali hiyo hiyo ya uchanga na utoto aliyo nayo, na kwa  nyimbo hizo, Yesu Kristo atazidi kujaa ndani yake katika umri huo huo alionao na utakua umepanda mbegu njema ndani yake na kwako utakuwa umetimiza neno linalosema.

Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Shalom.

Shea na Wazazi / Walezi wengine ujumbe huu.


Mada zinginezo:

Amepatwa na haya tangu lini?


JE! KUNA TOFAUTI GANI KATI YA MTU WA MUNGU NA MTOTO WA MUNGU?


MWANAMKE ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE, JE!  NI UZAZI UPI HUO UNAOZUNGUMZIWA?


MAMA MKWE WA KIKRISTO, JIFUNZE KITU KUTOKA KWA NAOMI.


JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *