FUNDISHO MAALUMU KWA MZAZI WA KIKE (MAMA KWE).
Kama wewe ni mama wa Kikristo, unaposoma maandiko kuna wanawake wengi sana ambao kwa kupitia ushuhuda wa maisha yao, kuna mengi ya kujifunza katika wakovu wako. Leo kwa neema za Bwana tumwangalia Naomi, ambaye wewe kama mama Mkristo mwenye wakwe (mabinti), utakuwa na kitu cha kujifunza kutoka kwake katika maisha yako ya wokovu. Lakini kwanza kabisa, hebu tumfahamu huyu Naomi.
Naomi alikuwa ni mke wa Elimeleki, mtu wa kabila la Yuda
Ruthu 1:1 Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili.
2 Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko.
3 Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili.
4 Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Wakakaa huko yapata miaka kumi.
5 Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.
Hapo tunaona Naomi baadae alikuja kufiwa na mume wake, lakini si hivyo tu, na watoto wake wote wawili ambao walikufa pasipo kuacha uzao wowote ule isipokuwa wake zao tu (Mabinti wawili ambao ni Ruthu na Opra). Sasa Naomi baada ya kuona hayo kuwa amefiwa na mumewe na watoto wake wakiume pia ambao waliacha wake, akaamua kuwaita hao mabinti wawili (wakwe zake), na kuwaagiza warudi kwa wazazi wao ma wawe huru kuolewa tena, wazae watoto na kuapata familia.
Lakini ukisoma habari hiyo utagundua kuwa, mabinti hao wote wawili walikataa bali walikusudia kwenda na Naomi mkewe wao
Ruthi 1:8 Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; Bwana na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.
9 Bwana na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia.
10 WAKAMWAMBIA, LA, SIVYO; LAKINI TUTARUDI PAMOJA NAWE KWA WATU WAKO.
Ila baada ya naomi kuwashurutisha sana ndipo Mmoja akarudi (ambaye ni Opra), lakini mwengine alikataa kabisa (ambaye ni Ruthi)
Ruthi 1:14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye.
Ninachokata uone hapo ni hiki, ulishawahi kujiuliza kwanini mabinti hao walimpenda sana mkwe wao? Na tena walikuwa tayari kuwa nae na kuambata nae katika nchi yake, ulishawahi kujiuliza ni kwanini? Kwa sababu katika hali ya kawaida sio kitu rahisi hata kidogo, jibu ni kwamba, upendo ambao alikuwa nao Naomi kwa mabinti hao (wakwe zake), ulikuwa ni mkubwa mno, na ndio uliowafanya na kuwavutia mabinti hao kukubali kuambata na mama wa waume zao, na zaidi ya hayo, Naomi alimcha Mungu na kuonesha upendo ambao uliwavutia hata mabinti hao.
Sasa swali ni je! Na wewe kama mama mkwe wa Kikristo, ni nini ambacho mabinti wa vijana wako wa kiume wanavutiwa na wewe? Je! Unamcha Mungu na kuwa na upendo kiasi cha kuwashawishi na kuwavutia wengine kuambata na Mungu Wako? Au wewe ndio unakuwa adui mkubwa wa wakwe zako?
Hivyo, kama wewe ni mama mkwe wa Kikristo huna budi kuwa na tabia hiyo kama ya naomi kusudi wengine wa vutwe na upole wako, na mwenendo wako wa upendo katika Kristo.
Bwana atusaidie,
Tafadhari shea na mama wakwe wengine wa kikristo ujumbe huu.
Mada zinginezo:
BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO
KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)
IFAHAMU HUDUMA YA MWANAMKE “MZEE “KATIKA KANISA.
MWANAMKE ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE, JE! NI UZAZI UPI HUO UNAOZUNGUMZIWA?
Msaidizi wa kufanana naye ni nani ambaye Mungu alimfanyia Adamu? (Mwanzo 2:18)