Shalom, jina la Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, karibu katika kujifunza neno la Mungu linalojenga roho zetu katika safari yetu fupi ya hapa duniani.
Sote tunafahamu kuwa, Mungu husema na kila mtu duniani kwa nyia nyingi na tofauti tofauti, Mungu husema na watakatifu kwa njia tofauti tofauti, husema na wenye dhambi kwa nyia nyingi mno, husema pia na watu walio na ulemavu wa akili, watoto n.k
Lakini moja wapo ya njia ambayo Mungu anayoitumia pia kusema na wanadamu (waouvu au watakatifu) ni pale tunapoamua mioyoni mwetu KUTAFAKARI HATIMA YA MAMBO TUNAYOYAFANYA JINSI YATAKAVYOKUWA. Tunapo zamilia kutafakari juu ya vitu tunavyovifanya hatima yake na jinsi itakavyokuwa, basi Mungu anaweza sema na sisi kwa kutumia nafasi hiyo ili kutujulisha ya mbeleni kisha sisi tufanye maamuzi wenyewe, kwa mfano; mtu anayeishi na mke au mume wa mtu akiamua moyoni mwake kutafari hatima ya hicho anachokifanya, Mungu anaweza sema nae huyo juu ya hatima ya hicho kitu kuwa ni mbaya kwa sababu Mungu hapendi huyo mtu apotee au kuaribikiwa, hivyo atamjulisha hatima ya hicho kitu kisha mtu mwenyewe atafanya uamuzi.
Hebu tumtazame mfalme Nebukadneza kwenye biblia, ambaye alidhamiria ndani ya moyo wake kutaka kufahamu hatima ya mambo yatakavyokuwa kwa vile alivyo, na Mungu akasema nae katika shauku yake hiyo na kumjulisha mambo yatakavyokuwa yaliyohusu matamanio yake.
Mfalme huyu wa dunia Nebkanzena, alikusudia moyoni mwake kutaka kufahamu hatima ya jinsi mambo yatakavyokuwa baadae kuhusu utawala, na Mungu kwa kufahamu nia yake hiyo, basi, akamjuza hatima ya mambo yote yaliyohusu ufalme wa dunia, alisema nae kwa njia ya ndoto juu ya kutaka kufahamu kwake, pengine mfalme alitafakari ni nani atakayetawala baada yangu, au kuna mfalme mwengine wa dunia atakayeinuka kaka mimi, au nani atakayetawalala milele na milele, na ndipo Mungu akasema nae juu ya tawala zote, kuanzia ufalme wake wa Babeli hadi utawala wa Yesu Kristo ambao utakaodumu milele na milele.
Lakini biblia inatuambia hayo yote aliyafahamu baada ya yeye kutaka kujua hatima ya mambo yajayo kuhusu ufalme na utawala na Mungu akasema nae.
Danieli 2:29 Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako YA MAMBO YATAKAYOKUWA HALAFU; na yeye afunuaye siri AMEKUJULISHA MAMBO YATAKAYOKUWA.
Hii inatufundisha nini na sisi? Hii Ni kutufundisha kuwa, endapo na sisi tukiamua kutia mawazo mioyoni mwetu, kutaka kujua juu ya mambo yatakayo kuwa kutoka na uasherati wetu tunaoufanya, Ulevi wetu, starehe na udunia tunaoupenda, umbea wetu na usengenyaji tunaoufanya, wizi na rushwa, kujichubua, mawigi kucha bandia, na make ups, kusujudia masanamu n.k Mungu atatujuza nini hatma yake, sasa kumbuka, Mungu anaweza asikujibubu kwa ndoto kama mfalme Nebkanzena, bali amaweza kukujibu kwa njia nyingine kama vile mahubiri ya mitandaoni, watu wanaokuhubiria mtaani kwako, marafiki n.k hivyo ukipata kujua hatima ya hivyo vyote basi usipuuzie bali chukua hatua.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Bwana akubariki, Shalom.
+255652274252/ +255789001312
Mada zinginezo:
Hamna haja kukujibu katika neno hili.
Je! Ni kweli majuma sabini aliyoambiwa Daniel yamekwisha timia?(Daniel 9:23-27)
Itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni.