FUNZO KUTOKA KATIKA KISA CHA NADABU NA ABIHU.

Biblia kwa kina, Uncategorized No Comments

Kama Kanisa la Mungu, lipo Jambo la muhimu sana tunalopaswa kujifunza kutoka katika kisa cha Nadabu na Abihu kwenye maandiko matakatifu, kwa sababu, kisa cha watu hao hakikuandikwa kwa bahati mbaya hata kidogo, bali kiliandiandikwa kwa lengo la  kutufundisha sisi yaani kanisa, ili kwa saburi na faraja ya hayo maandiko, tupate kuwa na tuamami kama biblia inavyosema katika.

Warumi 15:4 KWA KUWA YOTE YALIYOTANGULIA KUANDIKWA YALIANDIKWA ILI KUTUFUNDISHA SISIILI KWA SABURI NA FARAJA YA MAANDIKO TUPATE KUWA NA TUMAINI

Watu hawa Nadabu na Abihu, walikuwa ni miongoni mwa watoto wa Kuhani mkuu na wa kwanza wa kimwili katika taifa la Israeli ambaye ni Haruni.

Hesabu 3:2 Tena majina ya hao wana wa Haruni ni haya; NADABU mzaliwa wa kwanza, NA ABIHU, na Eleazari, na Ithamari. 

Lakini kitu cha pekee tunachokisoma kuhusu watoto hawa wa Kuhani mkuu Haruni ni kwamba, katika maisha yao ya utumishi, walifanikiwa KUMUONA MUNGU WA ISRAELI (ndivyo maandiko yanavyosema).

Kutoka 24:9 Ndipo akakwea juu, Musa, na haruni, NA NADABUNA ABIHU, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli; 

10 WAKAMWONA MUNGU WA ISRAELICHINI YA MIGUU YAKE PALIKUWA NA SAKAFU ILIYOFANYIZWA KWA YAKUTI SAMAWIKAMA ZILE MBINGU ZENYEWE KWA USAFI WAKE.

11 Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; NAO WAKAMWONA MUNGU, wakala na kunywa. 

(Kwa urefu wa habari hiyo unaweza soma kitabu hicho cha kutoka sura ya 24 yote)


Ijapokuwa Nadabu na Abihu watoto wa Kuhani mkuu Haruni walimwona Mungu wa Israeli, Aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, lakini siku walipoenda kinyume na maagizo ya Mungu Huyo kwa kusogeza mbele Zake moto wa kigeni ambao Yeye hakuuagiza, Nadabu na Abihu walikufa pale pale pasipo kujali kwamba walimwona Mungu wa Israeli.

Walawi 10:1 Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza.

2 Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, NAO WAKAFA MBELE ZA BWANA. 


HII INAFUNUA NINI KATIKA KANISA?


Na sisi pia Wote tuliomwamini Yesu Kristo na kubatizwa kwa jina lake sawasawa na (Matendo 2:38) ni watoto wa Kuhani Mkuu Ambaye Ni Yesu Kristo (Waebrania 3:1), na kama tu ilivyokuwa kwa Nadabu na Abihu jinsi walivyomwona Mungu wa Israeli, ndivyo ilivyo na kwa wengi wetu leo hii.


Wengi wetu tumemwona Mungu wa Israeli kwa namna mbali mbali na kwa namna tofauti tofauti, wapo ambao wamemwona Mungu kwa kusema nae kabisa katika maono n.k, wapo ambao wamemwona Mungu katika maisha yao akiwapigania na kuwatendea mambo makubwa, wapo waliomwona Mungu akiwatoa katika utumwa wa dhambi n.k, wapo waliomwona Mungu katika karama mbali mbali na vipawa mbali mbali, lakini hiyo hata siku moja isikufanye wewe mtoto wa Kuhani Yesu Kristo uende kinyume na yale ambayo Mungu ameyaagiza kama walivyofanya Nadabu na Abihu, kwani utaishia kukataliwa na kuangamizwa siku ile katika ziwa la moto. 


Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

FUNZO KATIKA HABARI YA MFALME AHABU NA NABII MIKAYA


FUNZO KATIKA HABARI YA DANIELI NA MAANDISHI YALIYOANDIKWA NA VIDOLE VYA MWANADAMU KATIKA UKUTA WA ENZI YA MFALME


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.


NA MANENO YA MANABII YAPATANA NA HAYO, KAMA ILIVYOANDIKWA.


VIVYO HIVYO WANAWAKE NA WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, PAMOJA NA ADABU NZURI, NA MOYO WA KIASI; SI KWA KUSUKA NYWELE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *