Neno konzi lina maana gani?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Konzi ni neno la vipimo linalomaanisha ujazo wa mkono. Kitu chochote kinachojaa katika mkono ni konzi..

Utalipata Neno hilo katika vifungu hivi;

Mhubiri 4:6
[6]Heri konzi moja pamoja na utulivu,
Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;
na kujilisha upepo.

Soma pia.

Isaya 40:12, Kutoka 9:8, Ezekieli 13:19, Walawi 2:2.

Kwamfano katika habari hiyo, Bwana anatushauri ni heri tupokee kipimo kimoja kidogo cha mkono lakini tuna amani na furaha mioyoni mwetu kuliko kupokea vipimo vingi na huku tuna machafuko, na huzuni.

Sehemu nyingine biblia inasema:

Mithali 15:16-17
[16]Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA;
Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.
[17]Chakula cha mboga penye mapendano;
Ni bora kuliko ng’ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.

Ni jambo la kawaida mwanadamu kukimbilia kutazama faida za nje tu..na kusahau hasara za ndani. Lakini hapa hekima inatufundisha tuchague kwanza yale mambo ambayo yanatupa amani, bila kujali ni vichache kiasi gani tunavipata katika kuchagua hivyo.

Hiyo ni hekima..

Leo hii utakutana na wimbi kubwa la watu wanakimbilia kazi ambazo ni mizigo kwao kisa tu zinawalipa mshahara mkubwa.

Wengine wanafanyishwa kazi hadi siku ya ibada..bila kupumzika mwezi mzima mwaka mzima..wengine wanaathiri mpaka vipindi vyao vya ibada za nyumbani kisa tu “ovetime” kazini.

Hii ni mbaya sana..tuwe watu wa kiridhika. Na Bwana atakuwa pamoja nasi.

Swali ni je! Umeokoka? Je unafahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na Yesu yupo mlangoni kurudi? Unyakuo ni wakati wowote, umejiwekaje tayari?

Majibu tunayo

Tubu dhambi zako ikiwa hujaokoka.

Shalom.

Bwana anatushauri tuthamini amani na utulivu kuliko faida kubwa.

Shalom

LEAVE A COMMENT