Fahamu maana ya mstari huu “Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.”

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu kupitia jina la Yesu karibu tujifunze neno la Mungu ..

Tusome

[2]Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.

Jambo tunanalopaswa kufahamu wanadamu wote waliopo duniani, aliyewaumba ni Mungu tu, hakuna mwanadamu ambaye amejiuweka mwenyewe hapa Duniani, kwahiyo hata haya makundi mawili ya tajiri na maskini yote ni Mali ya Mungu ..

Japo ni kweli tajiri humdharau maskini, kwa jinsi alivyo alivyo, na maskini pia huona wivu kwa tajiri, lakini mambo haya hayaondoi kusudi la Mungu, BABA yeye anajua wote aliwaumba yeye

Na ndiyo maana wanategemeana tajiri anamtegemea maskini na maskini anamtegemea tajiri, kwahiyo heshima ya tajiri ipo kwa sababu maskini yupo, kama kundi hili lisingekuwepo tusingejua kuwa kuna watu ni matajiri

Funzo ambalo Mungu anatupa sisi wanadamu ni kuwa ameruhusu makundi haya miwili, si kwa ajili ya kumpendelea tajiri na maskini ateseke, si kweli.. bali Mungu alitaka tuishi kwa upendo na amani kwa sababu sisi sote tu wa baba mmoja na tunategemeana, tajiri usiwe na dharau Wala wewe maskini usione wivu, ni kanuni ya Mungu, tudumu katika umoja

Bwana akubariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *