UFISADI NI NINI, NA UNAMAANISHA NINI KIBIBLIA?

  Uncategorized

JIBU…

Ufisadi kibiblia ni tofauti na jinsi watu wanavyoitafsiri, kikawaidia ufisadi unatafsirika kama kuhujumu uchumi wa nchi au shirika fulani

Lakini kibiblia ufisadi hautafsiriki hivyo
Ufisadi kibiblia unamweleza mtu mwenye tabia ya uzinzi na uasherati uliozidi kupita kiasi kwa maana nyingine kundi hili linajulikana kama makahaba au Malaya

Hivyo unapoona neno hili katika biblia moja kwa moja jua kabisa mwandishi alililenga kundi hili na siyo mtu anaye hujumu uchumi wa taifa fulani..

Tuone baadhi ya mistari ambayo inazungumzia kuhusu ufisadi

1 Petro 4:3
[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

[4]mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.

2 Petro 2:7
[7]akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;
Na mingine mingi .., lakini hiyo itoshe kujua jinsi ufisadi ulivyotafrika katika maandiko
..

Je mafisadi watakwenda mbinguni ?
Moja kwa moja, Jibu ni hapana sawa sawa na Neno la Mungu

Wagalatia 5:19-21

[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Hapa biblia imetoa maelezo ya kutosha kabisa hakikisho juu ya watu kama hao wafanyao ufisadi
Lakini hali hii hawezi kuondoka hivi hivi kama hujaruhusu maisha yako yatawalie na Roho Mtakatifu maana yeye pekee ndiye anatupa nguvu ya kushinda mambo yote ya mwili

Waefeso 5:16-18
[16]mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

[17]Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Sasa unawezaje kumpokea Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu unampokea kwa kutubu kwa kuzamilia kabisa ndani ya moyo wako kuasha maisha ya uovu, baada ya hapo unabatizwa, ubatizo wa maji mengi kwa jina la Yesu, baada ya kukamilisha hatua hizo hapo hapo Roho mtakatifu ataingia ndani yako na kuanza kukusaidia kushinda tamaa za mwili, kisha Furaha ya wokovu itazalika ndani yako nawe utaanza kumfurahia Mungu kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu bila shida

Je umekamilisha mambo hayo ikiwa bado basi ujachelewa wakati ni huu Bwana anakupenda ndiyo maana hata leo umeweza kuona habari hii, Mungu anakupenda na anataka ubadilike wewe ni mtoto wake, amekuandali mazuri zaidi ya haya unayoyaona hapa duniani

Matendo ya Mitume 2:37-40
[37]Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

[39]Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

[40]Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.

Bwana akubariki kwa kuchagua fungu..

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba hizi
+225693036618/ +225789001312

LEAVE A COMMENT