Mamajusi ni watu gani?

Maswali ya Biblia No Comments

Mamajusi, ni watu walitoka masharikii ya mbali maneno ya babeli na walikuwa watu ambao wanachunguza maandiko na walikuwa na shauku ya kumjua Mungu wa Israeli zaidi.

Pia hawakuwa wayahudi yaani Waisraeli, ndiyo maana maandiko yanasema walitoka masharikii ya mbali, katika biblia katika nyakati ilipozungumzia Mashariki ilikuwa Ina maanisha nchi za mbali mfano babeli au hidi

Tofauti na wanavyodhahaniwa kuwa walikuwa wasomo nyota na wachawi, hawakuwa watu wa jinsi hii, bali kutokana na bidii yao katika kumjua Mungu wa Israeli wakati wapo safari wakitafuta kwenda kujifunza zaidi ndipo walipewa ishara ya nyota ambayo iliwaongoza Hadi pale Bwana Yesu alipokuwa amezaliwa

Mathayo 2:1-2
[1]Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,

[2]Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

Hii ni tabia ya Mungu kwa wale wanaotafuta kwa bidii hiwap ishara mbalimbali, Hutumia ishara mbalimbali kuthibitisha jambo ambalo mtu yeyote alikuwa akilichunguza.

Japo kuna injili aua mafundisho yanayoharisha usomaji nyota hii si sawa na ni mafundisho ya uongo lazima tuwe makini katika hili

Nasi Leo tukiongeza bidii katika kumjua Mungu zaidi zipo ishara nyingi Mungu atatuonyesha, ambazo zitamfunua Yesu Kristo katika maisha yetu,

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *