Je kuvaa suluari kwa mwanamke ni dhambi?

Maswali ya Biblia No Comments

Kumekuwa na sintofahamu sana katika swala hili la uvaaji wa suluari, haswa kwa wanawake kuna baadhi ya watu, hudai kuwa ni vazi kama vazi lingine maana linamsitiri mwanamke, Je jambo hili ni kweli?

Jibu: Ukweli ni kwamba vazi hili suluari halimpasi kabisa mwanamke kuvaa, kwanza kabisa vazi hili la suluari tunalithibitisha katika maandiko lilionekana kuvaliwa na makuhani, na kama tunavyojua katika agano la kale makuhani walikuwa ni wanaume.

Kutoka 28:41 “Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.

42 Nawe wafanyie SURUALI ZA NGUO YA KITANI, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;

43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake”.

Kupitia maandiko haya yanatudhibitishia kuwa vazi hili lilikuwa maalumu kwa wanaume tu, ni vile tu watu wanavyopamba dhambi inapakwa rangi ili ionekane kuwa ni nzuri na wala haina madhara yeyote, hakuna m yummy 6ahali popote maandiko yamehalalisha kuwa kuna suluari za kike na za kiume, zaidi biblia imekanusha jambo hili katika maandiko

Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.

Suluari si vazi la mwanamke wala si vazi linalomsitiri badala yake ni vazi linamwaibisha mwanamke, maana mwanamke anapovaa suluari maungo yake yote huwa yanajionyesha wazi wazi hadi nakuwa ni aibu hata watu kumtazama, tofauti na mwanaume anapovaa inakuwa kawaida tu, kwa sababu kavaa vazi linalompasa na kwa mwanamke pia anapovaa sketi ndefu au gauni refu inakuwa kawaida tu kwa sababu kavaa vazi linalompasa avae

Hivyo basi suluari si vazi la kike usidanganyike kabisa, vitu vidogo vidogo kama hivi vinaweza kukukosesha mbele za Mungu kwa kushindwa kuweka utii kwake, maandiko yanasema kutii ni bora kuliko dhabihu, ikiwa Leo ndiyo umelitambua hili basi ni wakati wako wa kibadili mtazamo na kufata kile Mungu anataka ufanye

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *