Kufunga ndoa au harusi ni agizo la Mungu au ni mapokea ya wanadamu?.

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe.

Jibu: suala la kufunga ndoa lipo kibiblia kabisa ( ni Agizo la Mungu) lakini harusi ni karamu au sherehe tu kuadhimisha tukio Hilo la muhimu kati ya wahusika [Bibi na Bwana Harusi].
Sasa sherehe hizo huenda kulingana na Mila na Desturi za mahali husika.

Utaona pia Yesu katika mifano yake aliwahi pia kutumia mfano huu [Mfano wa wanawali 10]. Ilikuwa ni sehemu ya Desturi za kiyahudi..

Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

2. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.”

Kufanya sherehe wakati wa ndoa mpya hakuna dhambi hapo!
Kufanya sherehe au kutofanya sherehe wawili wanapofunga ndoa ni maamuzi huru kabisa, kikubwa tu yafanyike kwa maadili kama wafuasi kamili wa Yesu Kristo.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *