Kukaramkia maana yake ni nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mpendwa karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Turejee maneno ya Bwana kutoka katika kitabu hiki ili tuelewe zaidi neno linasema.

2Wakorintho 7:2 “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.

3 Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja”

Kukaramkia ni kitendo cha kutapeli ambapo mtu au watu hutumia maneno ya vinywa vyao kudanganya wengine ili wanufaike au wapate faida kutokana na udanganyifu wanaoufanya na udanganyifu huu hufanywa mara nyingi na manabii wa uongo wanaohubiri neno la Mungu kwa kupotosha ili wanufaike binafsi kifedha.

Inatupasa kuwa makini na manabii wa sasa kwakuwa wengi wao ni waongo hivyo tusiwape nafasi mioyoni mwetu kwa njia ya kulisoma neno la Mungu ambalo litatuongoza na litatupa ufahamu wa kujua manabii wa kweli na manabii wa uongo.

Neno la Bwana linasema.

Wafilipi 3:17 “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;

19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo

Hivyo inatupasa tuwahubirie watu kweli ili waokoke na kuacha dhambi na siyo kuitumia injili kwa lengo la kushibisha matumbo na kujiingizia pesa ya udhalimu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *