Shalom mwana wa Mungu karibu tena katika kujifunza.
Tukianzia sura hiyo ya 16 hadi 17 kuna jambo ambalo alilieleza Paulo hadi akasema yeye ameaminiwa uwakili tusome
1Wakorintho 9:16 “Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
17 Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili”.
Umeona hapo, anaelezea kuwa alipewa jukumu la kuihubiri injili na amewekewa sharti, ndiyo maana hapo akamaliza kwa kusema ole wake asipoihubiri injili
Ukweli ni kwamba Paulo, alijitoa sana kuifanya kazi ya Mungu kwa sababu alitambua nini kinachompasa kufanya, ndiyo maana Paulo aliichukua kazi ya Mungu kama mtu aliyeajiliwa, hivyo alikuwa yupo chini ya bosi wake, alikubali kutii alicho agizwa na kuzingatia yale anayopaswa afanye kwa uangalifu na kwa umakini mkubwa ili asiharibu kitu chochote.., ndiyo maana ya hiyo kauli aliyosema “nimeaminiwa uwakili” kuwa yupo kama muajiliwa chini ya mtu fulani.
Ndiyo maana tuona katika utumishi wake ni mtume wa kipekee aliyeta matokeo makubwa sana katika kazi ya Mungu
Tunaweza kuweka utofauti mkubwa kati ya mtu aliamua tu kufanya kazi fulani au kajitolea tu, tofauti inakuwa huyu anakuwa na uamuzi mkoni mwake anaweza kuamua kwenda au kutokwenda kwa sababu hakuna mtu aliye chini yake, ila yeye ana amua kufanya au kutofanya kabisa
Je ni nini tunajifunza kutoka kwa Mtume Paulo juu ya andiko hili?
Lakini nasi lipo jambo ambalo tunaweza kujifunza hapa, sisi nasi tumepewa uwakili katika kuifanya kazi ya Mungu, hivyo tunapaswa kunyenyekea sana na kufanya kwa umakini mkubwa, usiruhusu kabisa kuifanya kazi ya Mungu hadi uamue mwenyewe hapo wewe utakuwa si mtumwa wa Kristo, bali mtumwa wa dunia hii , lakini tambua kuwa sisi sote tumeandikiwa uwakili
Hivyo tunatakiwa kuifanya kazi ya Mungu Muda wowote na majira yoyote yale.. tukiwa tayari kwa wakati unaofaa na usiofaa.. tusiifanye kazi ya Mungu kwa kujisikia kuwa leo nina hamu ya kufanya kazi ya Mungu ndio unafanya lakini ukiwa huna hamu hufanyi si Kristo anavyotaka sisi tuwe.. tumeaminiwa uwakili..siku zote wakili analipwa na hafanyi kazi bure na sisi tujitowe sana kufanya kazi ya Mungu maana iko Thawabu kubwa tumeandaliwa baada ya kumaliza kazi yetu hapa duniani.
1 Wakorintho 4:1
[1]Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.
Hivyo sisi tu mawakili wa siri za Mungu.. tumeaminiwa na sisi pia tuwe waaminifu kwa mwajili wetu (Yesu Kristo) kwa kuihubiri siri hii (injili iletayo wokovu kwa watu wote bila kubagua wala kuangalia ni nani anatakiwa kuhubiriwa siri hii).
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.