Maana ya kuota una mimba

Ndoto No Comments

Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo. Karibu katika Maneno ya Uzima

Unapokosa uelewa kuhusu ndoto, kwanza utashindwa kutambua kusudi la Mungu juu ya hiyo, pia imewafanya wengi kuwa watumwa wa ndoto zao wakihisi Kila ndoto ni ya kuzingatia na Ina tafsiri Fulani tofauti. Lakini si hivyo!

Ukweli ni kwamba inabidi kwanza ujue makundi haya makuu matatu ya ndoto

> Ndoto zinazotokana na Mungu,

> Ndoto zinazotokana na Shetani, Na

> Ndoto zinazotokana na Mtu mwenyewe yaani mazingira yanayomzunguka, Shughuli anayoifanya kutwa, maisha ya Kila siku n.k

Ndoto kundi hili la tatu huwa hazina maana, maana ni mambo tu unayoyawaza Kila wakati. Huchukua sehemu kubwa mpaka Asilimia 95%. Na wengine wamekuwa watumwa wa Ndoto za namna hii kwa kukosa elimu yake, maana SI Kila ndoto Ina ujumbe wa muhimu kuufuata.

• KUOTA UNA MIMBA

Ikiwa ndoto hii imekuja bila sifa za zile ndoto kundi la tatu, yaani unaweza Kuta mwanamke amewaza sana kuhusu kupata mtoto, au amesikia habari Fulani kuhusu mimba, amemuona mwanamke akikatiza barabarani akiwa na mimba n.k na kujikuta usiku anaota ndoto ana mimba basi ndoto hiyo haitakuwa na maana. Lakini kama sivyo basi huo ni Ujumbe kutoka kwa Mungu.

Kama tunavyojua matunda ya mimba ni kitu Fulani kuzaliwa, haijalishi ilipatikana kwa njia halali ama sio halali ila ni lazima kiumbe kipya kizaliwe!.

Ikiwa ndoto hii imekujia zaidi ya mara moja basi uchukulie uzito maradufu, tunajifunza kwa habari ya farao aliota ndoto Ile ya miaka saba ya njaa na saba ya neema mara mbili na ndio ilimfanya kuona kuna uzito wa kujua maana yake.

Kwanza kabisa ni kupata matarajio yako ya muda mrefu mfano kitu umekuwa ukifanyia maombi kwa muda mrefu basi tarajia kukipata nyakati hizo mfano Sara alitarajia kupata mtoto na alitokewa na malaika nae akamwambia mwakani muda kama huu utalea mtoto. Mimba huja Kwa mbegu Fulani iliyopandwa hivyo ulipanda njema utavuna kilicho chema.

Vilevile ulipanda uovu basi utavuna Maovu (dhambi). Kama ulikuwa mchawi utavuna matunda ya uchawi wako, ulikuwa MLA Rushwa, Muasherati, mzinzi au tapeli jiandae kupata matunda yake karibuni

Tukisoma..

Yakobo 1:14-15

14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”

Pia..

Zaburi 7:14

“Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.”

Isaya 59:3-4

3 “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya.

4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.”

Hivyo kama bado upo katika dhambi, basi ni nafasi yako kumgeukia Kristo Leo! Anakuita Kabla mabaya yatarajiwayo hayajakufika. Mpe Leo rasmi maisha yako

Na kama umekuwa katika wokovu wako na umeomba Dua na Sala kwa ajili ya mambo mema basi tarajia mema katika njia zako.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *