“Maana ya kuota upo shuleni”

Ndoto No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo na Asifiwe

Ndoto za aina hii zimekuwa zikiotwa na Watu wengi kwa namna tofauti tofauti, mfano wengine wanaota wanafanya mitihani migumu sana kwao Lakini wenzao Wana uwezo wa kujibu isipokuwa wao tu, au anafanya mtihani na hawakujiandaa, au kimefika kipindi Cha mitihani wanagundua hakuna walichokifanya siku zote n.k

Namna nyingine ni watu kuota wapo madarasa Ambayo walishayavuka siku nyingi, au wanapewa adhabu, wengine wanaota wanafundishwa n.k kwa namna yoyote Ambayo unajikuta upo mazingira ya shuleni basi ni Ujumbe wenye maudhui sawa utokao kwa Mungu.

Ni aina ya ndoto zinazosumbua sana kutokana na kuota mara kwa mara { baada ya wiki au miezi} na wengine tofauti kulingana na mtu mwenyewe
Tukichukulia mfano kwa kitabu Cha Ayubu

Ayubu 33:14-15
14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”

Kutokana na fahamu zetu Mungu hupenda kutufundisha akitumia mifano ya vitu vinavyotuzunguka. Tunajifunza pia kwa mwanawe Yesu Kristo alipenda kutumia mifano kama wafanyabiashara, wakulima, Wafalme, Wanaharusi, familia n.k

Hivyo Mungu anapokuletea habari ya wokovu hutumia kile kitu kilichotukuka sana katika ufahamu wako ambacho ni muhimu, na unapokikosa basi umekosea Maisha nacho ni ELIMU

Hufunua kwamba ipo Elimu iliyo kuu, ufunguo wa maisha ya dunia hii na ijayo elimu hiyo ni elimu ya ufalme wa Mbinguni.

Maisha ya shuleni yanatumika kuonesha kiwango chako cha kiroho  Hivyobasi ni Mungu anasema nawe mfano kujiliwa na mitihani angali hukujiandaa, mitihani kuwa migumu n.k basi ndivyo ilivyo hali yako kiroho. Kuna madarasa hujayamaliza bado hivyo kiroho unashindwa kuendelea, unakwama japo unatamani kusogea mbele zaidi.
Unachopaswa kufanya ni kuongeza mahusiano yako na Mungu kwa kuomba na kusali sana, kujifunza na kutafakari Maandiko, kuishi maisha matakatifu kwa kupunguza muda wa kuhangaikia Dunia na kuongeza muda kwa Muumba wako, na huo ndio ufunguo wa maisha yako yaliyopo na yatakayokuja.
Ukimpata Mungu Umepata vyote, ndiposa Maandiko yanatuasa

Mathayo 6:33
” Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

Unapoonesha bidii kumtafuta Mungu kwa kiwango hicho hicho Mungu anajidhihirisha kwako na kukuvusha viwango vingine vya ufahamu wa kiroho. Hii inaonesha kiasi ambacho Mungu anakupenda kwa kusema nawe kupitia njozi hizo, Usipuuzie wito huo mpendwa Ongeza bidii!

Maranatha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *