Mbinguni kutakuwa ni kuimba wakati wote tu?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mpendwa karibu tujifunze maneno ya uzima toka kwa kristo mfalme.

Hakuna andiko linalosema na kuthibitisha kuwa mbinguni ni sehemu ya kuimba tu bali Bwana wetu yesu kristo alisema anaenda kutuandalia makao kama neno linavyosema.

Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.

Hapo amesema anaenda kutuandalia makao mengi na siyo machache na sehemu yenye makazi inashughuli nyingi.hivyo mbinguno ni sehemu yenye matukio mengi vinginevyo duniani ingekuwa nisehemu nzuri kuliko mbinguni.

Hii inamaana kuwa mbinguni ni mahali palipo changamka zaidi ukilinganisha na duniani ambapo vitu vya kutuchangamsha ikiwemo uimbaji lakini tutambue kuwa mbinguni ni zaidi ya duniani.
Zitakuwepo shughuli nyingi na mambo mengi yatakayotupatia Raha.

Ni mahali ambapo tutapata kumfurahia Mungu kwa viwango ambavyo hatujawahi kumfurahia.

Hivyo mbinguni siyo mahali pa kuimba tu wakati wote Bali yapo mambo mengi yatakayofanyika huko ambavyo biblia inasema ambavyo hatujawahi kuviona Wala sikio kisikia.

1Wakorintho 2:9 “ lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao”

Inatupasa kitafuta kwa bidii kuingia mbinguni kwa gharama zozote zile ili tusikose mambo mazuri aliyotuandlia mbinguni.
Na lango la kuingia mbinguni ni yesu krito biblia inasema.

1Wakorintho 2:9 “ lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao”
Na lango la Mbinguni ni Yaya pekee yesu kristo neno linasema.

Yohana 14:5 “Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?

6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”

Kwa kuungama dhambi zote na kubatizwa pia kwa ubatizo wa maji mengi na pia kwa kusoma biblia.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *