Mtu aliyeua anaweza kubeba dhambi za yule aliyemuua?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mpendwa katika kristo karibu tujifunze maneno ya uzima Toka kwa Bwana wetu yesu kristo.

Kama mtu atamkataa Mungu na ghafla akafa katika dhambi zake kwa kifo Cha aina yeyote iwe kuuawa, kupewa sumu n.k mtu huyo atazibeba dhambi zake mwenyewe na kwenda nazo anakostahili kwenda nazo Bali yule muuaji ataibeba dhambi ya uuaji na siyo dhambi za aliyeuawa.

Wagalatia 6: 5 “Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe

Kitu kimoja tu ambacho Mungu atamdai yule ambaye hatamuonya mwingine aiache njia yake mbaya. Na hicho siyo kingine Bali ni damu ya huyo mtu.

Ezekieli 3:18 “Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako”.

Nini maana ya kuwa na hatia ya damu ya mtu?

Hatia juu ya damu ya mtu sito kuzibeba dhambi zake maana yake ni kuwa na kila sababu za kuwajibishwa kwa kusababisha madhara kwa mwingine.maana yake kama haujamuonya aiache njia yake mbaya na ukizingatia ulikuwa na nafasi ya kumuambia aache mapema na yule mtu akafa pasipo kusikia maonyo yeyote basi adhabu itakuja juu Yako na wakati mwingine laana na hata kifo.

Katika Sheria za kawaida mtu aliyemuua mwenzake hachukui madeni yake Bali aliyemuua atahukumiwa kwa kosa la mauaji ambapo adhabu yake yaweza kuwa ni kifo hivyo aliyemuua mtu hatobeba dhambi za aliyemuua.

Hivyo tunajifunza kuwa makini hususani baada ya kuokolewa ni wajibu wako kupeleka injili kwa wengine ili damu isiwe juu yako kama mtume Paulo alivyosema

Matendo 20:25 “Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.

26 Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote.

27 Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu

Kuipeleka injili Siyo kuongea tu Bali hata kuchangia pia kazi ya Mungu ni kuipeleka injili pia.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *