Mwandishi wa kitabu cha mathayo ni nani?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo na Asifiwe

Mwandishi wa kitabu Cha mathayo. JE ni nani?

Jina la kitabu lajieleza lenyewe “INJILI KAMA ILIVYOANDIKWA NA MATHAYO MTAKATIFU” kuonesha Mwandishi ni Mathayo, Sasa swali linakuja, Je! Ni mathayo yupi?

Biblia haijaeleza moja kwa moja kuwa ni yupi, lakini wanazuoni wengi na watafiti wa historia ya biblia wanahitimisha kuwa ni Mathayo Mtume wa Yesu, Yule mtoza Ushuru, Ambaye Katika luka 2:14 Anatajwa kwa Jina la Lawi.

Kitabu hiki kinaelezea Mwanzo wa kutokea kwake Mwokozi duniani, Maisha yake, kifo chake na kufufuka kwake.

Pia utakuta vitu kama historia yake, Miujiza aliyotenda pamoja na hotuba zake, Ambazo zipo kuu tano nazo ni

1. Hotuba ya mlimani (Mathayo 5-7)

2. Hotuba ya utume (Mathayo 10)

3. Hotuba ya ufalme wa mbinguni (Mathayo 13)

4. Hotuba ya kanisa (Mathayo 18)

5. Hotuba ya Siku za mwisho (Mathayo 24)

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *