Je dia ni nini kibiblia
Maana ya neno dia, kwa maana nyingine linatafsirika kama “fidia” tusome kifungu hicho hili tuelewe vizuri nini maana halisi ya neno hilo
Mithali 13:8 “Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”.
Kwahiyo hapo tunaweza kusema “faida ya nafsi ya mtu ni utajiri wake ” mfano tutolee katika maisha ya kawaida tu, mra nyingi mtu mwenye pesa, ikiwa atafanya kosa fulani au kusababisha hasara ya jambo Fulani, sasa pesa zake huyo mtu ndiyo huwa fiidia kwa ajili ya hivyo vitu alivyovitia hasara, au anaweza kuvamiwa na majambazi kisha wale watu wakaanza kumtishia uhai wake, hapo hawezi kujitetea na jambo lingine zaidi sana atatoa pesa zake ziwe fidia ya uhai wake
Lakini ukiendelea mbele hapo kwenye hilo andiko anaendela kwa kusema
Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”.
Kwa maskini huwa tofauti kidogo, huwezi kukuta maskini anapokea mashutumu ya namna hiyo, au hawezi kuvamiwa ni majambazi kwa ajili ya kitaka mali zake huwa ngumu, ndiyo maana hapo anamalizia kusema hasikii ogofyo kwamba hawezi sikia matisho yeyote
Tunajifunza nini hapa
Ipo hekima tunaweza kujifunza hapa, siyo kwamba ni makosa kuwa tajiri au ili uwe salama, bora uwe maskini, jibu ni la kuwa maskini au tajiri haiwezi leta Kinga bora maishani mwako, Bali anayetupa hakikisho la maisha yetu kuwa salama ni Yesu Kristo tu
Lakini hekima tunayo ipata hapa hata kama una pesa nyingi ishi maisha ya wastani tu usitake Kila mtu atambue kuwa wewe ni mtu mwenye pesa nyingi, kama ukiishi maisha ya namna hii yatakufanya uwe na amani
Mithali 13:7 “Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”
Kuishi maisha ya kutokujionyesha kama pesa si dhambi ishi kawaida tu kama wengine, usijbague, sisi sote tu wamoja.
Ubarikiwe..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.