Nini maana ya sakitu(Ayubu 38:29)

Maswali ya Biblia No Comments

 

Nakusalimu katika Jina la Bwana Yesu Kristo.

SAKITU ama kwa lugha ya kiingereza “Frost”. Ni barafu iangukayo kutoka juu ifunikayo uso wa ardhi, mimea n.k hasa katika nchi au maeneo yenye baridi Kali.

tusome..
Ayubu 38: 29 “Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na SAKITU YA MBINGUNI ni nani aliyeizaa?

30 Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi”.

Biblia imeonesha hili pia katika Kutoka 16:14, Tunaona pia kuwa hata Ile MANA ilifanana na SAKITU kimwonekano, lakini haikuwa sakitu.

Tukisoma kutoka 16:14,15


Kutoka 16:14 “Na ulipoinuka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama SAKITU juu ya nchi.

15 Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao Bwana amewapa ninyi, mle”

MANA ilifananishwa na SAKITU kwa baadhi ya tabia zake, Mfano kuyeyuka baada ya kupigwa na jua, sifa iliyopo katika Sakitu pia.

Tuangalie tena..


Kutoka 16:21 “Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na hapo jua lilipokuwa ni kali, kikayeyuka”.

Maranatha.

Usisahau kuwashirikisha wengine habari hizi njema kwa kushea

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *