Utukufu halisi wa mana

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo

Wana wa Israeli walipokuwa jangwani Walipewa mana, lakini haikuwa na Ubora sawa, japokuwa ni mana ileile. Sasa ni kivipi?

Majibu tunayapata kitabu Cha kutoka 16:19-36..

1. Kulikuwa na Mana iliyodumu siku moja

Hii iliokotwa kila asubuhi, na kupikwa na iliyeyuka baada ya kupigwa na jua. Tunasoma pia kuwa iliposazwa mpaka siku ya pili ilivunda.

2. Ya pili ni Mana iliyodumu kwa siku mbili (2).

Mungu aliwaangiza hii Siku moja kabla ya sabato, yaani iliwe mpaka siku ya sabato na itakuwa sawa tu haitavunda. Itavunda kama ikisazwa Hadi siku ya tatu.

3. Ya tatu ni Mana iliyodumu Daima.

Haikuharibika hata vizazi vyote. Ni Ile Musa aliyoagizwa aiweke ndani ya sanduku la Agano, iwe kumbukumbu hata vizazi vyote.

Kuna ufunuo Gani Nyuma ya Hilo katika Agano jipya?

Mana ni chakula walichopewa na Mungu wale wangali Jangwani, na hawakupasuka miguu Wala kuugua.

Hata kwetu leo Mana ni chakula Cha kiroho tulichopewa tuliomwamini, tule angali tupo katika Dunia hii ya uovu, kusudi katika hicho tusiathiriwe na dhambi mpaka Ile siku ya ukombozi wetu itakapofika.

Chakula hicho ni ufunuo wa Yesu Kristo au “NENO LA MUNGU LILILOFUNULIWA” (Yohana 6:30-35)

Mtu aliyeokoka anapaswa kujifunza Neno Kila siku ili aukulie Wokovu wake kama Israeli walivyokula mana Jangwani. Hii huja Kwa mafundisho sahihi na kusoma Biblia Kila siku. Wapo wengine husema hatuna haja ya kujihangaisha “Yesu alimaliza yote pale msalabani” huu ni Upotovu mkubwa

Kiroho mtu huyu huonekana anakula mana, lakini ya mwamzoni ni inayomtia nguvu kwa kitambo kidogo tu. Mfano mtoto anakunywa maziwa tu, lakini wewe u akula ugali, Wote mnakula! Lakini vyakula vina nguvu tofauti. Ni hivyo pia kwa mwongofu mpya hupewa mafunuo ya awali yaani maziwa.

Nazo fadhili za Mungu zitakuwa nae jinsi anavyoendelea kukua siku hata siku kwa kufundishwa na kujisomea. Mwongofu mpya asiposoma, kufundishwa, kujifunza kwa muda mrefu ni rahisi sana kufa Kiroho. Hivyo kujipima Imani au kiwango chako Cha kiroho angalia Usomaji au kujifunza kwako Neno la Mungu.

MANA YA PILI.

Lakini kwa kadri mwongofu anapojifunza na kuwa karibu zaidi na Mungu, basi lile neno linapokea nguvu ya kulihufadhi kwa muda mrefu kidogo. Wana wa Israel walipoingia katika Sabato na Mungu wao ili kumsifu na kumwabudu basi Ile MANA yao haikuvunda.

Fadhili za Mungu hukaa juu yao wamtumkiao na kumfanyia Ibada kwa Moyo wa dhati. Mtu akipunguza ukaribu wake na Mungu au kupoa katika wokovu hakika atashuhudia Nguvu za Mungu zikipunguka ndani yake, uzito utaamka tena (Ukame).

Mfano wa mana atakayopewa mtu huyu; ni mithili ya kile chakula alichopewa Eliya na malaika, Ile nguvu ya kile chakula ilidumu kwa miaka arobaini.

MANA YA TATU.

Hii hudumu milele, lakini sharti lake ni moja {ikae ndani ya Sanduku}. Nasi Leo sanduku letu ni Yesu Kristo.

Wakolosai 2:3 ” ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.”

Kwa kadri unavyoendelea kumtumikia Bwana kwa Uaminifu na kwa muda mrefu, basi naye Bwana Atajifunua kwako, Naam Fadhili zake hazitakoma hata Milele! Kwasababu UMEUFIKIA ule Utakatifu halisi wa Mana iliyofichwa Ambayo SI Kila Mtu hufikia.

Hali huu humfanya mtu kuwa chini ya fadhili na Neema za Mungu, hatarudi Nyuma Tena, Wala hatapoa Kiroho, Mungu Atajifunua kwake kwa namna ya kipekee..

Kama alivyosema na kanisa la Pergamo katika Ufunuo 2:17

[17]”Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. YEYE ASHINDAYE NITAMPA BAADHI YA ILE MANA ILIYOFICHWA, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.”

Nini maana ya Kushinda?

Tukisoma kuanzia mstari wa 12 anasisitiza uaminifu, kutokuikana Imani, kutokujichanganya na Mafundisho ya Uongo yatakayokudumaza Kiroho. Mfano ni Balaamu alivyowaletea Waisrael wanawake WA kimataifa wawaoe ili wawafundishe kuabudu miungu, ili tu awafarakanishe na Mungu wao!

Basi mpendwa epuka Mafundisho ya Dunia, Baki kwenye njia ikufanyayo kuwa Mtakatifu. Jua kwamba mana imefichwa katika sanduku, unapaswa wewe kuingia humo kuifikia, kwa maisha Matakatifu ya kumtii Yesu Kristo Bwana wetu.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *