Shalom. Karibu tujifunze Biblia
JIBU: Kwa majibu turejee katika Maandiko
Wafilipi 3:2
” Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.”
Hapa tunakutana na makundi matatu hatari ya kujihadhari nayo “Mbwa” pili “Watendao mabaya” tatu ” Wajikatao”
Sasa tutalitazama kila kundi kati ya haya tukianza na makundi mawili ya mwisho
[Kundi la Kwanza]”Watendao mabaya” Hawa ni wenzetu katika Imani lakini ni watenda mabaya na biblia inatuonya tusichangamane nao, Na Biblia inaliweka hili vizuri kupitia mtume Paulo
1 Wakorintho 5:9-11
9″ Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.”
Na lengo kuu kutochangamana na Watu watenda mabaya
katika kanisa ni ili wajisikie aibu, Wageuke na kutubu.
[Kundi la pili] ” Wajikatao ” watu wamekuwa wakichanganya kati ya ” Wajikatao” na wajikataao ni makundi mawili tofauti kabisa. Biblia inapozungumzia Wajikatao hawa ni wayahudi wanao shinikiza tohara ikiwa ni njia pekee ya kukubaliwa na Mungu
Kulikuwako na hata sasa lipo kundi la waamini wanaosisitiza tohara kama jambo la lazima kwa Mungu, na mtu asipotahiriwa hawezi kukubalika na Mungu..Kundi hili walimwamini Yesu lakini bado Sheria za torati ziliwaendesha, Ambazo kimsingi haziwezi kumkamilisha mtu Mbele za Mungu isipokuwa Yesu pekee.
Hata kushika siku, mwezi, mwaka, sabato hayafai kumkamilisha mtu bali neno la Mungu.
Tusome..
1 Wakorintho 7:19-20
19″ Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa.”
[Kundi la tatu] “Mbwa” Sasa JE Hawa Mbwa ni kina nani?
Bwana Yesu alikwisha kuwataja Hawa Mbwa ni kina nani
Tusome..
Mathayo 7:15-16
15 “Jihadharini na MANABII WA UONGO, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni MBWA-MWITU WAKALI.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?”
Ni kama tunavyoona “Mbwa” wanaozungumziwa hapa ni ” Manabii wa Uongo” isiwe kidogo hawatajwi kama Mbwa tu Bali mbwa-mwitu wakali!! Tena wasiohurumia kanisa
Na hutawatambua kwa mionekano yao maana nje wamevaa mavazi ya Kondoo(wanafanana na watumishi wa kweli wa Mungu) lakini kwa Yale wanayoyaishi na kuyafundisha tutawatambua, Naam tutawatambua kwa matunda yao
Neno Manabii wa Uongo ni la jumla, yaani likijumuisha Wachungaji wa Uongo, waimbaji wa Uongo, waalimu wa Uongo
Kwa kifupi ni wote wanaosimama kuitangaza injili ya kristo angali maisha yao ya ndani si wakristo, Wanasifika kama watumishi wa Mungu ukiwatazama kwa nje.
Ikiwa mtu awaye yote akisimama kuihubiri injili nyingine tofauti na iliyoko katika biblia yaani injili ya wokovu, na kumfanya mtu afurahie dhambi badala ya kutubu mtu huyo kibiblia ni ” MBWA” na tumeonywa na tujiepushe nao
Naye nabii wa kweli atakuwa kama Musa! Akiwaelekeza watu wote kwa Mungu na si kwake Wala kwa miungu/shetani
Kumbukumbu la Torati 13:1-4
1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.”
JE! Unaongozwa na Miujiza, Ishara za maajabu, Nabii wa Uongo Au Neno la Mungu?
Kumbuka Maandiko yanatuasa
Kumbukumbu la Torati 6:4-5
4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.”
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.