Shalom.
Habari hii utaipata katika injili ya Luka 21:18 na mathayo 10:30,
Mathayo 10:30 ”lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote”
Luka akaandika hivi…
Luka 21:18 “Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.”
Ikiwa ni kuonesha kuwa hakuja kuleta ukombozi wa Roho pekee bali na hata miili yetu pia. Mtume Paulo anaandika kuwa miili hii ya uharibifu itabadilishwa kuwa ya kutoharibika..
1Wakoritho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 MAANA SHARTI HUU UHARIBIKAO UVAE KUTOKUHARIBIKA, NAO HUU WA KUFA UVAE KUTOKUFA.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?”
Tunaweza kuona pia anaposema Lakini ninyi hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu, ni dhahiri kuwa wapo watakaovipoteza vitu hivyo, ndio wale wanaokataa au kutokumwamini Yesu kama Kristo au masihi kuwa watapoteza au watahukumiwa. Hiyo itakuwa kama wakifa katika dhambi zao basi hatma yao itakuwa ni katika ziwa la moto wa kiberiti.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.