Tusome hapa..
Mathayo 14:23 “Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; MAANA UPEPO ULIKUWA WA MBISHO.
25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu”.
Biblia inaposema upepo ulikuwa wa mbisho maana yake ni upepo ulikuwa wa ukinzani, yaani ulikuwa unavuma kinyume na sehemu waliyokuwa wanaielekea..
Aina hii ya upepo ilionekana tena katika kitabu cha Matendo ya mitume..
Matendo 27:4 ”Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana PEPO ZILIKUWA ZA MBISHO”.
Watu wanaposafiri safari ya majini wakakutana na pepo za mbisho basi safari yao huwa ngumu sana kwa sababu upepo utakuwa unavuma kinyume na kile chombo walichopanda na kusababisha chombo kurudi nyuma hivyo lazima watachelewa kufika…
Kiroho ni nini?
Kiroho pepo za mbisho ni matatizo, dhiki, shida na kila aina ya vikwazo kutoka kwa ibilisi ambavyo hukwamisha maisha yetu ya imani. Tunaona wanafunzi wa Yesu walitaka kwenda nchi ya Wagerasi kwa ajili ya kufanya huduma ya kuponya wagonjwa na kufundisha lakini adui alituma upepo wa mbisho ili kuwazuia lakini baada ya Bwana Yesu kuingia katika chombo chao ule upepo ukatulia hii ilimaanisha huo ulikua mpango wa adui (Mathayo 14:23-36)
Jambo hili linatufundisha kuwa tunapokutana na pepo za mbisho basi yatupasa kuzikemea kwa jina la Yesu zitakoma wala hazitatuzuia.
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.