Yesu Kristo anatuombeaje kule mbinguni?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo.

Warumi 8:34

“Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; TENA NDIYE ANAYETUOMBEA.”

Ni dhahiri Bwana wetu Yesu Kristo ndiye Anayetuombea, soma Tena..

1 Yohana 2:1 “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi TUNAYE MWOMBEZI KWA BABA, Yesu Kristo mwenye haki,”

Angalia, Ili kupata Ujumbe kutoka kwa daktari basi ujue lugha ya kidaktari, hivyo hivyo kwa wanasheria, wanasiasa n.k Sasa hata kupata Ujumbe kwenye Biblia inatupasa kuijua na kuielewa Lugha ya Mungu au ya Kiroho.

Mfano Bwana Yesu alisema ” Mtu asipoula mwili wangu na kunywa damu yangu Hana Uzima ndani yake(Yohana 6:53)

Usipoielewa lugha inayotumika hapo utajikuta unafanana na wachawi na waganga.

Lakini unapoelewa kwamba alikuwa akimaanisha ule MKATE na kile KIKOMBE (Mathayo 26:26-27) Unaenda sawa sawa na Maandiko yanavyosema.

Sasa kwa ufafanuzi huo turejee katika Andiko letu la Leo Warumi 8:34 Unaosema Bwana Yesu ndiye anayetuombea kwa Baba, Sasa turejee mistari ya nyuma kidogo 26,27

Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA KWA kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”

Mstari wa 34 Unasema Bwana Yesu ndiye Anayetuombea; Mstari wa 26 unasema Roho Mtakatifu ndiye Anayetuombea, Sasa ni yupi Anayetuombea Yesu ama Roho?

Majibu mazuri tunayapata 2 Wakorintho 3:17 na hapo Ndipo kilipo kiini Cha somo letu

2 Wakorintho 3:17 “Basi ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.”

Maandiko yanasema Bwana Yesu ndiye Roho Mtakatifu;

Mfano tukiangalia Kitabu Cha Ufunuo sura ya 2 na 3 Ujumbe unaanza na YESU ANASEMA inamalizia na ROHO AYAAMBIA MAKANISA. Hivyobasi ROHO MTAKATIFU NDIYE BWANA.

Roho mtakatifu akiomba ni Bwana Ameomba.

Swali la mwisho kama Bwana ndiye Roho mtakatifu, JE Roho mtakatifu Anatuombeaje? Kama tunavyoona katika mstari wa 26?

Bwana (Roho Mtakatifu) Anaomba ndani yetu, si sawa na vile sisi tunavyoombeana!

Sisi tunapoomba basi Yale Maombi yetu anayachukua na kuyawasilisha mbele za Baba, kwa Lugha na maelezo mazuri zaidi.

Lakini haimaanishi anatuombea sisi tukiwa tumelala au tunacheza, au kufanya mambo yetu mengine, La! si kwa maana hiyo.

Hivyobasi Bwana wetu Yesu Kristo anatuombea kwa jinsi ya Roho Mtakatifu, nae Roho Mtakatifu Huchukua Maombi yetu na kuyawasilisha kwa Baba katika lugha Kamilifu Zaidi.

Si kweli kabisa kwamba Bwana Yesu anaomba, na kusali Mbinguni kwa Baba usiku na Mchana kwa ajili yetu, Bali ni kwamba hutuombea kupitia Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu.

Kumekuwa na Mafundisho ya Ibilisi makanisani yanayotuambia kwamba hatuna haja ya kujihangaisha kusali angali Bwana anatuombea Mbinguni usiku na Mchana, huo ni UPOTOVU mkubwa! Kutoka kwa adui shetani.

Tusipoomba sisi Roho mtakatifu hawezi kuomba, maana Roho mtakatifu ni kipaza sauti chetu mbele za Baba hivyo ni lazima Ufanye Maombi wewe kwanza.( Rejea somo la jinsi Roho anavyotuombea)

Kwa kuhitimisha tungependa kukutaarifu kuwa hakuna Mtakatifu aliyekufa Wala kunyakuliwa kwenda Mbinguni na kutuombea sisi Bali ni YESU KRISTO pekee kupitia Roho mtakatifu. Wala SI Eliya, henoko, mariamu, Rita Wala yeyote aliye hai au aliyekufa!

Cha msingi kwetu ni kumtafuta sana Roho mtakatifu ambaye kwa huyo Maombi yetu yanafika na kukubaliwa, na asiye na Roho Mtakatifu basi hiyo si wa Kristo ( Warumi 8:9).

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *