Fahamu tafsiri ya sifa na lami (kutoka2:3)

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Kuhusu jibu la sifa na LAMI ni Nini kama inavyotumika katika Kutoka 2:3, turejee 

Kutoka 2:3 “Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka SIFA NA LAMI, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto”

Sifa ni aina ya nta inayopatikana au kuzalishwa na aidha mimea au mafuta na hupatikana katika Mashina ya miti, lakini sifa inayozungumziwa si ile ya “Utukufu” au “kusifu”

Nta ya sifa ni Ile inayopatikana katika mabaki ya Makaa ya mawe ambayo huwa nyepesi kuliko Lami.

Lami hupatikana katika uhalisia wake maeneo ya bahari ya chumvi au SIDIMU mipakani mwa mto Yordani huko Israel.

Mwanzo 14:10 “Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa MASHIMO YA LAMI. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani”

Kimwonekano lami ni nzito kuliko sifa, ingawa rangi zake hufanana yaani zote ni Nyeusi.

Biblia inatabiri siku ya kisasi cha Mungu (ya mwisho) dhidi ya wanadamu Watendao maovu, Dunia itapigwa kwa moto Uunguzao, vijito na ardhi yote itakuwa lami.

Isaya 34:8 “Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.

9 Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, NA ARDHI YAKE ITAKUWA LAMI IWAKAYO”.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *