Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu tujifunze Maneno ya Uzima.

Mungu aliupenda Ulimwengu kwa sababu asili ya Mungu wetu ni UPENDO,
tusome..

1Yohana 4:16 ” Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. MUNGU NI UPENDO, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.”

Lakini si kwamba Mungu aliupenda Ulimwengu na mambo yake au mifumo, kazi Au Maovu yake, La! Tena alizikemea vikali (Yohana 7:7), Bali Mungu aliwapenda walio Ulimwenguni yaani Wanadamu, bila Upendeleo wa jinsia, rangi, taifa Wala matendo, Bali wote, Tulipendwa sawa!
Na upendo huu ulidhihirika katika Hali yetu ya Upotovu.

Kipindi tulichokuwa chini ya utawala wa mwovu Shetani, pasipo na  tumaini lolote, bila Uzima wa milele ndani yetu. Lakini kwa upendo wake Mungu mwenyewe akatuhurumia, ndipo alipotujilia ili kutuokoa kutoka Hali yetu ya kifo na Mauti, Bure!

Mungu wetu aliingia gharama, kwa Kumtoa mwana wake wa pekee Yesu Kristo ili aje katika hali ya mwili wa kibinadamu, afe kwa dhambi zetu kama fidia, ili kwa kifo chake yeye sisi tupone na mauti, hatimae tupokee uzima wa milele.

Na mtu yeyote atakayeukubali wokovu huo, ambao ni kufa na kufufuka kwake, Basi mtu huyo yu na uzima wa milele, na hiyo ndiyo maana ya andiko hili katika Biblia

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Lakini pamoja na kuwa uzima umeletwa kwetu bure, kwa gharama kubwa! Wapo wasioukubali!
Wakisema waweza kushinda uovu wa Ulimwengu huu kwa nguvu zao (kwa dini ,matendo yao Wenyewe)

Yohana 3:19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.”

Vipi kuhusu wewe Ndugu, JE! Umeupokea Uzima wa milele?
Ikiwa bado wakati ni sasa mpokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wako, mfuate kwa moyo wako wote, Uepukane na Dunia hii ya kitambo kidogo, inapita! Na haujui sekunde chache zinazokuja mbele utakuwa na hali gani..

Ikiwa upo tayari kuokoka Leo, basi utawsslia nasi kwenye mawasiliano yetu hapo chini

Ubarikiwe sana.

Usisahau kuwashirikisha wengine habari hizi njema kwa kushea.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *