Nini maana ya agano la chumvi? (2M.nyakati.13;5)

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze neno la Mungu.

Agano la chumvi ni Agano Gani kama inavyotumika katika 2Nyakati 13:5,

Turejee..
2Nyakati 13:5 “Je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa AGANO LA CHUMVI”

Neno hili linaonekana mara tatu katika Biblia Hesabu 18:19, 2Nyakati 13:5 na Walawi2:13

Sasa swali linakuja Nini maana ya Agano la chumvi?

Hapo zamani, na hata sasa katika baadhi ya maeneo chumvi mbali na kuwa kiungo cha kutia ladha katika chakula, pia hutumika kama kiungo vcha kuhifadhia vyakula vibichi/vikavu au ambavyo havijapikwa ili visiharibike au vidumu kwa muda mrefu.

Tunaweza kusema chumvi pekee ndio  AGANO BORA la kufanya kitu kisiharibike na kidumu kwa muda mrefu.
Ndio maana zamani katika Agano la kale sadaka zote (za unga na za wanyama) ziliwekwa chumvi kudhihirisha uthabiti wa Agano la Mungu

Walawi 2:13 “Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga UTALITIA CHUMVI; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote”.

Pia tukisoma katika kitabu Cha Ezekiel..

Ezekieli 43:22 “Na siku ya pili utamtoa beberu mkamilifu awe sadaka ya dhambi; nao wataisafisha madhabahu, kama walivyoisafisha kwa ng’ombe huyo.

23 Utakapokwisha kuitakasa, utatoa ng’ombe mume mchanga mkamilifu, na kondoo mume wa kundini mkamilifu.

24 Nawe utawaleta karibu mbele za Bwana, na MAKUHANI WATAMWAGA CHUMVI JUU YAO, nao watawatoa wawe sadaka za kuteketezwa kwa Bwana”.

Hivyobasi hapana shaka kwamba kilichodumu kwa muda mrefu kimetiwa chumvi nyingi. Kuna msemo unawatambua wakongwe kama “watu waliokula chumvi nyingi”. Biblia pia huwakilisha wakongwe kuwa wana chumvi nyingi mwilini mwao,

Ezra 4:11 “Hii ndiyo nakili ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta;watumishi wako,watu walio ng`ambo ya mto wakadhalika.

12 Ijulikane kwa mfalme ya kuwa Wayahudi, waliokwea kutoka kwako, wamefika kwetu Yerusalemu; nao wanaujenga ule mji mwasi, mbaya; wamemaliza kuta zake, na kuitengeneza misingi yake.

13 Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.

14 Na sisi, KWA KUWA TUNAKULA CHUMVI YA NYUMBA YA MFALME, wala si wajibu wetu kumwona mfalme akivunjiwa heshima, basi tumetuma watu na kumwarifu mfalme”.

Sasa turejee katika mstari wetu

2Nyakati 13:5 unaosema “Je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa AGANO LA CHUMVI”.

Ni dhahiri kwamba Agano la Mungu na Daudi kuwa atampatia ufalme ni Agano thabiti lenye kudumu milele lisiloharibika, kama chakula kile kilichotiwa chumvi.

Nasi Leo tunapomwamini Yesu, kutubu na kuziacha dhambi zetu basi Tunakuwa chumvi kiroho ambayo inatusaidia kudumu milele katika ahadi za Mungu na uzima wa milele.

Tunatiwaje chumvi ili tuweze kupata Uzima wa milele?

Marko 9:49 “Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”.

Nao moto huo ni Roho mtakatifu (Mathayo 3:11 na Matendo 2:3)

Ambao ukishuka katika maisha ya mtu huchoma Kila kilicho Cha kidunia na kushikamana na Maisha ya mtu huyo, wakati ni kwa maumivu kwa kuondolewa vile viungo vinavyomkosesha.

Na baada ya hapo huitwa kiumbe kipya, mwenye Uzima wa milele; na Hilo ndilo Agano la chumvi kwetu.

Umetiwa chumvi? Utakapomkubali Yesu kuwa Bwana kwako utakuwa Umetiwa chumvi na Roho mtakatifu, nawe utaitwa chumvi ya dunia(Mathayo 5:13) mwenye uhakika na maisha yako ya milele, hivyobasi ni vyema ufanye hivo Leo kama bado?

Na Mungu atakubariki sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *