“Heri asiye keti barazani pa wenye mizaha” mstari huu unamaanisha nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe!

Swali: Ni mizaha Gani inayoongelewa zaburi 1:1? Kuna tofauti kati ya mizaha na utani? Kama hamna utofauti, je? Hata kutaniana na mtu ni dhambi?

Jibu: tusome..

Zaburi 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha”.

Imezungumzia kwenda, kusimama na kuketi barazani pao, Maandiko haya yanakataza katika namna zote tatu. Tuangalie kwa undani zaidi kuhusu kifungu hiki, kwa kuangalia makundi tusiyopaswa kuongozana au kuambatana nayo..

1. Watu wasio HAKI

Hawa ni wale wasio na habari kabisa na Mungu [Ungodly], Watendao maovu na machukizo bila kujali wala kuwa na hofu na Mungu.

2. Wakosaji

Hawa ni wavunjao amri au sheria za Mungu kwa makusudi (wanaweza kuwa ni wakristo) lakini matendo Maovu kama uasherati, wizi, Ulevi na ufiraji n.k vinaambatana nao.

3. Watu wenye Mizaha

Ni kundi la hatari zaidi, ni wanaoleta mizaha na dhihaka katika mambo ya kiroho, kukejeli habari za wokovu, ufufuo n.k. Wengine utawaona katika majukwaa au mikusanyiko ya watu wakifanyia dhihaka maneno ya Mungu, Manabii na Ahadi za Mungu n.k

Mtume Petro anawatambua na kutuonya dhidi ya watu Hawa pia..

2Petro 3:3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,

4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa”.

Hivyo ni vyema kuwa macho dhidi kundi hili la hatari.

Utofauti kati ya mizaha na utani

Mizaha na utani ni maneno yanayoendana sana hata kwa kiingereza huitwa jina moja yaani ‘jokes’. Tukiwa kama Wakristo tunapaswa kuwa  waangalifu na wenye kiasi katika masuala ya mizaha, yaani yasifanyike kuhusu neno la Mungu, na pia yasivuke miiko ya maadili husika.

1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”

Kuepuka mizaha iliyopitiliza pia ni ushindi dhidi ya uasherati na uzinzi unaotokana na mizaha, pamoja na uongo ambavyo vyote hujifunika chini ya kivuli cha mizaha.

Mithali 26:19 “Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, JE! SIKUFANYA MZAHA TU?”

Kuwa  na kiasi katika Mambo yote, na kuzipenda Sheria za Bwana tutaepuka Maovu yote yanayotokana na mizaha isiyo utaratibu na kupita kiasi..

Mithali 19:29 “Hukumu zimewekwa tayari KWA WENYE MZAHA; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu”

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *