Rangi saba zilizo katika upinde wa mvua zinafunua nini?

Maswali ya Biblia 1 Comment

Shalom.

Najua ushawahi kujiuliza ni kwa Nini Kila nchi Ina bendera zenye rangi mbalimbali, ambapo Kila rangi huwakilisha kitu fulani mfano Tanzania ina rangi nne [Bluu, kijani, Nyeusi na njano]. Kila moja inawakilisha jambo fulani kuhusu Tanzania, ambalo litamjulisha Mtu kulihusu kabla hata hajafika..

> Kijani: uoto wa asili

> Bluu: Bahari na vyanzo vingine vya maji

> Njano: madini

> Nyeusi: wazawa au wananchi.

Mungu pia anayo bendera yake aliyoionyesha kwetu baada tu ya lile gharika kuisha, bendera hiyo ni Upinde wa mvua wenye rangi Saba, Inayojichora juu katika anga. Hiyo humwonesha Mungu ni nani kwetu.

Mungu wetu ana sifa mbalimbali kutokana na muktadha [Mazingira] tofauti, Mungu ni Mwingi wa Hasira [kwa wanaofanya uadui nae] mfano( Nahumu 1:2), na mwingi wa Huruma (Kutoka 34:6, Zaburi 145:8, Yoeli 2:13, Yona 4:2). Kwa ufupi ni kuwa Mungu ni Mwingi wa Hasira, lakini si mwepesi wa Hasira na hughairi Mabaya.

Tukirudi katika rangi, Rangi nyekundu huashiria moto, ghadhabu au Hasira. Kinyume Cha moto au nyekundu ni maji au Barafu yaani utulivu.

Vivo hivyo na rangi ya Bluu huwakilisha utulivu au Amani, upole au kutuliza. Hii ni rangi ya rehema au kinyume Cha rangi Nyekundu. Sasa mpaka hapo utakuwa umeanza kuelewa ni kwanini upinde wa mvua unaanza na rangi Nyekundu, Ile nyekundu huanza kufifia kufikia rangi ya chungwa (Orange) Kisha njano Kisha kijani. Hii inaonesha hasira ya Mungu hupungua kutoka juu kufika mpaka chini kabisa yaani Bluu na hatimaye kutoa Neema au Rehema badala ya Ghadhabu.

Utaona neema ya Mungu inazidi kuwa kubwa kuelekea kwenye rangi ya Bluu ikimaanisha utulivu wa Mungu na neema zinavyozidi kuwa nyingi, na hata kuipoza Ile ghadhabu kabisa.

Hivyo zile rangi Saba zinawakilisha ghadhabu ya Mungu jinsi inavyosogea na hata kuwa Rehema nyingi. Tunaona hata baada ya Nuhu kutoka kwenye gharika, Mungu alirehemu Tena Dunia iliyoharibika kwa gharika lile, na kuahidi kutokuiangamiza Tena kwa Maji( ghadhabu kutoka nyekundu kurudi mpaka kuwa Bluu).

Pamoja na hasira lakini MUNGU WETU anazo sifa nyingi za kuonesha jinsi alivyo na upendo na Wingi wa Huruma.

Pia anasema..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”

Sikiliza ndugu, upendo wa Mungu hauhesabu mabaya, haukumbuki ya nyuma, haijalishi Umefanya dhambi kubwa kiasi Gani maishani mwako, yeye anakuita Leo umgeukie yeye kwa kumwamini Yesu Kristo, na kumkabidhi maisha yako na kuacha dhambi zako kwa dhati kabisa [Toba].

Kisha ukabatizwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, upokee kipawa Cha Roho Mtakatifu nawe utahesabiwa haki Bure na hakutakuwa na hukumu ya adhabu kwako. Naye hatokumbuka kabisa uovu wako wa Zamani..

Zaburi 103:12

12 “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.”

Achana na maisha ya dhambi kwa moyo kabisa Wala si kwa hofu, mgeukie Mungu naye hatokuacha katika wokovu wako hata Milele.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

One Reply to “Rangi saba zilizo katika upinde wa mvua zinafunua nini?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *