nini maana ya mstari huu” Haiwezekani kuwafanya tena upya hata wakatubu”

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe nakusalimu kupitia jina la Yesu, karibu tena katika kujifunza neno la Mungu…

Tusome,

Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,

5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,

6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri”.

Katika Kifungu hiki “haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; maandiko yalikuwa yanlnawalenga watu ambao tayari amejua umuhimu wa wokovu katika maisha yake, na si hivyo tu na akapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, sasa maandiko yanamtaja mtu kama huyu endapo itatokea akaicha Imani, na kurudia mambo aliyokuwa anyafanya nyuma ndipo maandiko yanasema haiwezekani kuwafanya upya tena na wakatubu

Ikiwa na maana kuwa, si kwamba watu wa aina hii kama wakaiomba toba mbele za Mungu, haiwezeni wakasemehewa hapana si hivyo, bali neno la Mungu lilikuwa linamaanisha kuwa nguvu ya TOBA ndani ya mtu huyo inaondoka, yaani moyo wa toba unakuwa haupo tena ndani yake kwa sababu hii nguvu haiji tu, bali ni Roho Mtakatifu ndiyo anafanya kazi yake, sasa ikiwa kama atahudhunishwa ndipo hapo ile nguvu ya kuomba Rehema mbele za Mungu inakuwa haipo, ndipo hapo Kila kitu huwa kinaonekana sawa kwa mtu wa namna hii.

Hii ni alam kwa kila mtu anayepokea nguvu za Roho Mtakatifu, lipo anguko endapo pale unapoarudia vitu vya huko nyuma ni kuwa makini sana ikiwa kuna baadhi ya tabia za zamani umeona zimeanza kurudi hapo hapo.anza kukataaa hali hizi

2 Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa

22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”.

Basi ikiwa kuna baadhi ya vitu ambavyo huko nyuma ambavyo umeviacha, kisha ukaanza kuvipemba kama, uzinzi, uasherati, uongo, wivu nk.. ili uweze kulitatua tatizo hili ni lazima mambo haya usikubadli kuyarudia yale ya nyuma ni hatari.sana…..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *