Kumuita Mariamu mama wa Mungu ni sawa ?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze maneno ya uzima Toka kwa Bwana wetu yesu kristo.

Jibu ni hili kwamba mariamu alimzaa Bwana Yesu kwa namna ya mwili, hivyo wakati Bwana alipokuwa duniani  Mariamu alijulikana kama mama wa Yesu, na siyo mama wa Mungu.

Bwana yesu alipokuja hapa duniani alikuwa ni Mungu katika mwili lakini hakuja kutafuta kuabudiwa na ndiyo maana hakuna sehemu yeyote alijiita yeye ni Mungu, zaidi sana alikuwa anawarudisha watu wamwabudu Baba. Kumbuka Mungu alipouvaa mwili ilimpasa afananishwe na mwanadamu kwa namna zote azaliwe,ale chakula,asikie maumivu,alie,aone huruma na mambo mengine kama wanayoyatenda binadamu wengine siyo ajabu kumuona ikiwa na Baba,bibi,Babu au mjomba,lakini haimaanishi kuwa eye Yesu yupo chini ya hao wote.

Biblia anaelezea vizuri haya yote katika kitabu hiki kilicho katika neno la Mungu.

Mathayo 22:41 neno la Bwana linasema” Na mafarisayo walipokusanyika,yesu aliwauliza akisema,mwaonaje katika habari za kristo?

Mathayo 22:42 inasema” Ni mwana wa nani? wakamwambia ni mwana wa daudi.

Mathayo 22:43 inasema”akawauliza imekuwaje basi daudi katika Roho kumwita Bwana akisema.

Mathayo 22:44 inasema Bwana alimwambia Bwana wangu, uketi mkono wangu wa kuume, hata niwawekapo adui zako kuwa chini Yako?

Mathayo 22:45 inasema” Basi, daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

Wala hakuweza mtu kumjibu neno; Wala hakuthubutu mtu yeyote tangu siku Ile kumwuliza neno Tena”

Hapo jibu ka Mariamu litakuwa kwamba yesu atakuwaje mwanae na wakati Bado ni mwana wake? Na yeye binti wa Mungu (kwasababu kama daudi alikuwa mkubwa kuliko Mariamu aliambiwa hivyo je! Siyo zaidi yeye?

Hivyo sisi sote tunaomwamini Yesu kristo mbele zake ni ndugu na dada na yeye akiwa Baba yetu. Kwahiyo tujue ni muhimu kutofautisha jinsi Mungu anavyotenda kazi katika ofisi zake tofauti, Mungu anapoonyesha unyenyekevu (kuzaliwa kama mwanadamu).

Haimaanishi kuwa mwanadamu yupo juu yake hapa anafanya hivyo kutuonyesha njia iliyo Bora zaidi kama watoto wake.

Barikiwa na Bwana

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *