Fahamu tofauti kati ya dhambi, kosa, na uovu

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze maneno ya uzima.

DHAMBI,  Ni yale mambo yaliyokuwa yanafanyika kinyume na torati au sheria ya Mungu.
Ikimaanisha kuwa mtu yeyote aliyekuwa ameivunja hiyo sheria ni sawa na kutenda dhambi au ameiasi Sheria.
Ilijulikana kuwa mtu huyo kabla hajaiasi Sheria alikuwa anajua kabisa kuwa jambo Hilo lilisha hakikishwa na kuonekana kuwa ni kosa na mtu huyo alistahili adhabu Kali kwakuwa amefaanya kosa kwa kukusudia hata kulitia unajisi jina la Bwana kwa maovu.

MAOVU, ni mambo ambayo hayatakiwi kuwepo hapa ni yale mambo ambayo mtu anayafanya akijua kuwa ni kosa na ni uovu mbele za Bwana lakini mtu anafanya kwa makusudi huku nafsi ikiugua NDANI yake na kumjulisha analolitenda halimpendezi Mungu lakini mtu anakuwa anaendelea kufanya huo uovu hivyohivyo na maovu hupelekea hasira ya Bwana kudhihirika hata kupelekea kuadhibiwa na Bwana kama kipindi kile Cha sodoma na gomora.ulikuwa ni wakati ambao watu hawakuijua torati ya Bwana. Tunasoma

Mwanzo 6: 5 “Bwana akaona ya kuwa MAOVU ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.”

Kwhiyo mfano wa mambo yaliyokuwa yametendeka kipindi kile mpaka yakapelekea mji kuteketezwa kwa moto ndiyo yaliyotabiriwa kutokea katika siku za mwisho kwamba maovu mengi yataongezeka.

Leo hii tunaona mabaya mengi yanaongezeka na yamezidi Yale yaliyoandikwa katika biblia kama utoaji mimba, uvutaji sigara, uvataji wa madawa ya kulevya n.k haya yote yanajulikana kuwa ni makosa na sasa ni maovu.

KOSA, Ni sawa na kutofanya inavyostahili.mfano mtu anaposema “nimekosea” inamaana ametenda isivyostahili.tukisoma neno linasema

Matendo 2:38 ” ….Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Mtu anapoenda kumnyunyizia maji kichwani kama ishara ya ubatizo na kuepuka ubatizo wa maji ya kuzamishwa na akatumia jina linguine ambalo siyo jina la Yesu kristo kubatiza Hilo hujulikana kuwa ni kosa

Hivyo mkristo ili usiwe mtu mwenye makosa na mawaa yeyote mbele za Mungu, unapaswa uepuke yote matatu yaani DHAMBI, MAOVU, na MAKOSA. Na haya yote tunaweza kuyaepuka ikiwa utaliishi na kulifanya neno la Mungu kuwa msingi pekee wa kuyaendesha maisha Yako.

Dumu katika maandiko matakatifu ya Mungu huku ukimwomba Mungu akufunulie njia sahihi ya kuiendea huku ukitia Nia hiyo kwa kumaanisha roho mtakatifu mwenyewe atakuongoza na mwisho wa siku utajikuta unakuwa mwanawali mwerevu ambaye Bwana wake siku akifika atamkuta huku taa yake ikiwa imejaa mafuta kama inavyoelezwa kwenye mathayo 25.

Dunia imejaa maovu ya kila namna usiruhusu uchikuliwe na namna ya Dunia hii

warumi 12:2, hivyo mkristo ili uwe mtu asiye na HILA, MAWAA, na MAKOSA mbele za Mungu unatakiwa uepuke mambo haya yaani MAKOSA, DHAMBI, na MAOVU na haya utaweza kuyaepuka ikiwa utaliishi na kulifanya neno la Mungu kuwa ndiyo msingi na mwongozo wa maisha Yako.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *