Tofauti kati ya Mbinguni, peponi, kuzimu na jehanamu

Maswali ya Biblia No Comments

 

MBINGUNI

Maeneo mengi ya biblia yanaposema Mbinguni huwa yanamaanisha ni moja kwa moja kule Mungu alipo, anapokaa pamoja na malaika zake, ndipo huko Bwana Yesu alipokwenda kutuandalia makao, ambao kwa sisi watu wa Mungu, watakatifu bado hatujafika hata mmoja wetu..

Hiyo Ndio mbingu ya tatu ambayo alinyakuliwa mtume Paulo na kuonyeshwa vitu ambavyo kibinadamu haviwezi kuelezeka, kwasababu upeo wa akili zetu bado ni mdogo..(2Wakorintho 12:1-4)

Ni viwango vya juu zaidi ambavyo huwezi kuvielezea,au kutoa Maelezo yenye kutosheleza mpaka pale tutakapokwenda na kushuhudia kwa macho..

2Nyakati 6:18 “Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga!”

PEPONI/ PARADISO

Hii ni sehemu ya mangojeo,tunaweza kuiita mbingu ya mangojeo kwasababu sio makazi ya kudumu, Mtakatifu wa Mungu anapokufa anakwenda kwenye hii sehemu ya paradiso akingoja siku ya unyakuo ifike, auchukue mwili wake Katika kaburi na kisha aungane na wale watakatifu walio hai kwa wakati huo na wote pamoja wataungana kwenda Mbinguni kwa Bwana Yesu alipo mwenyewe.. haleluya

Pale msalabani, Bwana Yesu alimwambia yule mwizi neno hili..

Luka 23:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.

43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.

Ikijulikana kama mbingu ya pili au mangojeo, kwa jina lolotell lile, lakini kiujumla ni sehemu ya mangojeo kwa watakatifu, wakati mwingine biblia imetumia kifuani mwa Ibrahimu, kule lazaro maskini alipokuwa (Luka 16:19-31) ndio huko pia zilipo zile roho chini ya madhabahu zikilia na kuomba kulipiziwa kisasi kwa waliowatesa..

Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.

Na ndo huko pia wale wafu waliofufuka na Bwana walipoelekea kwa mara yao ya kwanza.(Mathayo 27:52-53)

Ukifa katika Kristo moja kwa moja unakwenda kwenye sehemu hii nzuri ya mangojeo ukingoja ufufuo wa mwisho..

KUZIMU

Ni sehemu ya inayomaanisha makao ya wafu, au kwa lugha nyingine kaburini, huko walikuwa wanakwenda wema na waovu kabla ya Kristo kuja katika ulimwengu na kuwatenganisha makao yao,

Ayubu 14:13 “Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!”

Mfalme Daudi alilisema hili, zaburi 16:10, Bwana hatomwacha huko milele..

Baada ya Bwana Yesu kuja watakatifu walitoka makaburini na kwenda paradiso, mahali penye raha ya juu sio makaburini, kwa kuwa watakaobaki huko ni wale waovu..

JEHANAMU

Sehemu hi ni mangojeo pa wafu, ni sehemu yenye mateso, kama tu paradiso palivyo na raha kwa watakatifu, hivyo na jehanamu ni mangojeo ya wafu waovu wanaokufa sasa, wakiendelea kuadhibiwa huko na kungoja siku ya hukumu ifike, ni katika hukumu ya kile kiti cheupe cha Mwanakondoo, wakatupwe kwenye ziwa la moto,ndiyo mauti ya pili..

Ni mwizi amekamatwa kwenye uwizi wake, kabla hajahukumiwa kufungwa, atapelekwa mahabusu akisubiri siku ya kupandishwa kizimbani ifike,ili apokee hukumu yake ya kuhukumiwa kwenda jela, sasa hivyo ndivyo ilivyo kwa wafu wanaokufa nyakati hizi na waliokufa zamani, sehemu yao ni hapo penye mateso makali..

Bwana anasema..

Marko 9:45

[45]Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [

JIULIZE MAKAO YAKO NI WAPI?

Embu tafakari ujiulize,ukifa leo au unyakuo ukikukuta utakuwa upande upi ndugu, vitu ambavyo huwezi kuvichukulia kwa wepesi ni maisha yako ya milele, ukshaondoka duniani hauna nafasi ya pili tena ya kutubu, ikiwa utaenda jehanamu basi ni huko huko milele..

Mgeukie Kristo Leo,mkabidhi maisha yako kwa kutubu kwa kumaanisha kabisa na kuuacha ulimwengu na mambo yake maovu,

Tubu dhambi zako maanisha kumfuata Kristo

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *