Watu wenye kuvunja maagano ni watu wa namna Gani?(Warumi 1:31).

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mpendwa karibu tujifunze maneno Bwana ya uzima.

Neno la Bwana linasema

Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,

30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,

31 wasio na ufahamu, WENYE KUVUNJA MAAGANO, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;

32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”.

kwenye

Watu wanaovunja maagano ni watu ambao hudumu katika ahadi zao.

1.wanaovunja maagano ya Imani

Mtu anapookoka anakuwa ameingia agano la Damu ya yesu

Mtu anapoamua kuuacha wokovu na kuyarudia matendo yake ya nyuma maana yake amevunja agano la damu ya yesu.

Tunaweza kusoma.maandiko haya ya Bwana

Waebrania 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 Mwaonaje? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”

2.Agano la ndoa

Ni agano ambalo linahusisha mwanamke na mwanaume pale wanapokusanyika wapo watu wengi kanisani agano linalohusisha viapo vya kuishi milele katika shida na Raha n.k

Ikitokea wameachana na mmoja wao akaoa au kuolewa hapo wanahesabika kuwa wamevunja maagano.

Ikiwa umeoa au kuolewa tambua haupaswi kuachana na huyo aliyekuoa au kuolewa naye kwakuwa mmefunga maagano mazito kanisani.

3.Agano lako mwenyewe

Ni nadhiri inayofungwa kati ya Mungu na mtu kwaajili ya muda.

Tusome maandiko haya.

Mhubiri 5:4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.

5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe”

Ikiwa umepanga kulifanya jambo jema inakupasa ulitimize.

Kwa upande wa mhubiri huyu aliyetokewa na Bwana kwenye maono Bwana akamwambia.

“Kama hutakuwa mwaminifu katika maneno yako mwenyewe, basi huwezi kuwa mwaminifu katika maneno yangu”.

Akimaanisha kuwa kama umepanga kufunga au kuomba halafu katika roho haujatekeleza unaonekana ni mtu uliyekosa uaminifu hata kwa mambo yako binafsi.

Yakobo 1:7 “Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote”.

Kumbukumbu 23:23 “Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako”.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *